GET /api/v0.1/hansard/entries/604933/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 604933,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/604933/?format=api",
    "text_counter": 12,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kajiado na watu wa Makueni wameshakaa kuongea kuhusu shida ya mpaka. Kama kuna shida iliyotokea, hiyo ililetwa na Kenya Gazette ya 1992 wakati nchi yetu ilibadilisha mfumo wa kisiasa wa chama kimoja na kuwa na demokrasia ya vyama vingi. Wakati huo, miji mingi yetu ilikuwa ikifurahia demokrasia ambayo ilikuwa imepatikana. Watu wengi, hasa wale ambao walikuwa wakikifuata chama kilichokuwa kikitawala, walipatwa na uoga wakiogopa kwamba demokrasia ambayo ilikuwa imekuja ingewatoa uongozini. Kwa sababu hiyo, walienda kwa tume ambayo inasimamia uchaguzi na kubadilisha jiji la Emali kuwa upande wa Makueni. Sultan Hamud pia iliwekwa upande wa Makueni. Baadaye, tulijua mpaka wetu ulikuwa ni reli. Pale Sultan Hamud, watu wetu walijua mpaka wetu ni reli. Wacha niseme wazi kwamba hakuna mji wetu katika Kajiado Kaunti ulijipata ukiwa mji bila idhini ya watu wetu. Mbeleni tulikuwa na mashamba ya vikundi. Wakati vichaka vilianza kukatwakatwa na watu wakaanza kumilika mashamba, sehemu fulani zilitengwa kama miji. Miji ya Emali na Sultan Hamud upande wa Kajiado zilibuniwa kutoka kwa mashamba ya vikundi. Kuna mashamba ambayo hadi leo yana vyeti vya umiliki ambavyo vinaonyesha kwamba mipaka yake ni reli. Nikisema hivyo, tuna Mbunge ambaye ni wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Madam Pareno, ambaye shamba la baba yake mpaka wake ni reli. Ukifuatilia mambo ya mashamba ya vikundi, utapata mambo haya ni sawa. Chifu wa kwanza wa Kajiado, ofisi yake ilikuwa Emali. Vyeti ambavyo ni vya kumiliki mashamba katika sehemu hiyo vilikuwa vikitolewa na Kajiado County Council. Naomba Sen. Mutula Kilozo Jnr., ingawa maombi yake ni mazuri, tuangalie mambo haya kwa makini sana. Hii ni kwa sababu watu wetu wa Emali kutoka Ukambani na kutoka Kajiado hawajawahi kuwa na shida za mpaka. Hakuna mpaka ambao umeshahamishwa. Hatujawahi sikia hayo."
}