GET /api/v0.1/hansard/entries/604935/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 604935,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/604935/?format=api",
"text_counter": 14,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mositet",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 608,
"legal_name": "Peter Korinko Mositet",
"slug": "peter-korinko-mositet"
},
"content": "Bw. Spika, nimesema hivyo kwa sababu najua ni njia gani Seneta anataka kupitia. Tayari tuna shida nyingi za mipaka katika nchi yetu. Ningemuomba mhe. Seneta Mutula Kilonzo Jnir. Kwanza tubuni sheria za mipaka. Hii ni kwa sababu mizozo ya mipaka nchini Kenya imeleta utata sana. Ningependa Serikali Kuu ihakikishe imebuni kamati maalum ambayo itajumuisha watu ambao walikuwa wakuu wa mikoa na maofisa wa tume ya uchaguzi. Pia tunaweza kuwahusisha maofisa wa Tume ya Swazuri ambayo inahusika na kuangalia mambo ya historia kuhusu ugavi wa ardhi hapa nchini. Baada ya hayo, tuwape siku 90 ili waweze kutupa jawabu kuhusu utata huo wa mipaka. Hivi sasa, ningependa kuwaambia watu wa Emali na wale wa Makueni wakae kwa amani. Amani ndio imewafikisha pahali walipo na wazianzishe vita vyovyote vile kwa sababu ya mipaka ya kaunti hizi mbili. Bw. Spika, kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}