GET /api/v0.1/hansard/entries/605257/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 605257,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/605257/?format=api",
    "text_counter": 336,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "au hata tuzungumze nini, tayari makosa yamefanyika. Kama Biblia inavyosema, pahali umeangukia ndipo unapotakiwa kurudi pale uinukie pale, usimame tena uanze mwendo wako. Nchi hii imelia. Katika miaka ya ukoloni, Hayati Mzee Jomo Kenyatta na wenzake walipigania ukombozi wa taifa hili. Kenyatta alikuwa na mwito mmoja wa kusema “uhuru wa mwafrika”. Lakini Ngei alikuwa pembeni; Kenyatta alisema “Uhuru” naye Ngei akasema “na mashamba ya Mwafrika, Uhuru na mashamba ya Mwafrika.” Tegemeo la wananchi wa Kenya kutoka siku za enzi hzio ilikuwa kupigana na kujikomboa. Jambo la kwanza lilikuwa ni kupata mashamba ya Mwafrika baada ya Uhuru. Lakini badala ya utawala wa Hayati Kenyatta kuweka mashamba mikononi ya wale walioyapigania, aliyarudisha kwa Wazungu na yale yalibaki yeye na wenzake wakayakalia na Mwafrika akaachwa akiumia na akakosa njia. Katika siasa ya Hayati Kenyatta, aliwahidi Wakenya katika kitabu chake cha siasa kwamba kila nyumba katika taifa la Kenya itakuwa na maji ya mferejei itakapofika mwaka wa 2000. Tuliangalia na kutembea juu ya shida katika ya miaka hiyo yote mpaka mwaka wa 2000 lakini badala ya kuwa na maji ya mfereji katika nyumba zetu, maji yalienda zaidi ya kilomita 50 kutoka mahali yalikuwa zamani. Bw. Spika wa Muda, uongozi wa mheshimiwa Moi akiwa katika ile Serikali iliyounda Serikali ya kwanza, ulisahau ya kwamba Wakenya walipigania Uhuru ili wapate mashamba, wasomeshe watoto wao, wapate matibabu ya kufaa, barabara na mahitaji mengine. Majukumu manne yalikuwa lazima kwa Wakenya. Kama Serikali ya kwanza ya Kenyatta ingewapa Wakenya wakereketwa waliopigania Uhuru mashamba, shida ingetatuliwa. Kama wangewapa wananchi wetu maji wengeweza kulima, kupata chakula na kulipa kodi. Pia, wangeweza kuwasomesha watoto wao na kujenga hospitali zao na leo hatungekuwa pahali tuko. Lakini kwa sababu ya watu wenye vitambi vikubwa ambao walifikiria maslahi yao wenyewe, walitafuna wakiwa wachache lakini leo ninawaambia kwamba watavuna walichopanda. Sasa hivi kabila la Degodia na lile la Gare wanapigana na watu tisa wameuawa. Tunawapa pole wenzetu kule lakini huu ni mwanzo wa uongozi mbaya. Tutaendelea kuwatafuta wale ambao waliwaibia Wakenya, wasifikiri watakaa kwa amani, watakuwa watumwa katika nyumba zao. Hawezi kutembea bila askari wa kuwalinda. Askari wetu wamekuwa ovyo, wanapigwa pamoja na wale wanaowalinda kwa sababu hakuna mpangilio. Mheshimiwa Spika wa Muda, tulipitisha Katiba mpya ya Serikali ya ugatuzi ili tujikomboe baada ya Uhuru kwani hakuna chochote kizuri kilichopatikina na tukadhani kwamba ugatuzi utatusaidia. Sasa tuko katika mwaka wa tatu tangu tuanze mfumo wa ugatuzi. Lakini ugatuzi ulikuwa ni kupindua mwenendo wa Serikali Kuu kutoka tujinyakulie Uhuru mpaka leo ili maendeleo yaende mashinani. Cha kuhuzunisha hivi leo ni kwamba kaunti ninayoiwakilisha ya Machakos - tutizame hesabu ya pesa hizi; nasikia ya kwamba Seneta Boni anafanya hesabu vizuri sana lakini hata pesa zinazopelekwa katika kaunti ya Kiambu, hakuna uhakika kwamba zitafanya kazi ambayo zimetengewa. Sasa imekuwa ni pata shika. Nilimwona Rais akitabasamu apowasilisha Bungeni orodha ya majina ya watu ambao wanatuhumiwa kuhusika na ufisadi na kusema kwamba The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}