GET /api/v0.1/hansard/entries/605259/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 605259,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/605259/?format=api",
"text_counter": 338,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "amefaulu. Amewahi kuwakamata wezi wote ilhali hadi leo ni Kamau peke yake ambaye amefikishwa mahakamani? Hata mimi nilikuwa katika ile orodha lakini hadi leo sijafikishwa kortini. Nashangaa! Je, tabasamu ya Rais ilikuwa ni kwa sababu ya kubeba karatasi? Wewe ni mtu wa kubeba karatasi na kutabasamu au wewe ni mtu wa kutoa amri na amri hiyo itekelezwe? Ndugu yangu, Mheshimiwa Orengo, Senior Counsel aliitwa pale, tuliandamana naye hadi makao makuu ya EACC. Tulisikiliza mashtaka dhidi yake, hatukupata hata kosa moja na aliruhusiwa kurudi nyumbani Shida ni kwamba, Serikali yote kuu ina vitengo vya kutosha ilhali haviwezi kuwakamata wezi wanaoiba pesa za Serikali. Hivi leo tunashangaa kuona kwamba shamba la Karen – mimi, Mheshimiwa Orengo na Mheshimiwa Khalwale tulipelekwa kortini kwa sababu ya kusema kwamba tunawajua wahusika na kuyataja majina yao. Leo ukweli unadhihirika kama mchana jua likitua katikati, Tobiko anasema kwamba Mheshimiwa Ngilu apelekwe kortini lakini hapelekwi kortini kwa kuiba, anapelekwa kwa sababu ya kutajataja majina ya wale ambao alisema kwamba nyuma yake kuna majina ambayo atayataja nyuma ya majina mengine na dunia itatetemeka. Bw. Spika wa Muda, ukiangalia vita dhidi ya rushwa na magendo hivi leo, hakuna pahali inaenda. Katika mgao huu wa Bajeti, Kaunti ya Machakos ilipata Ksh6 bilioni na kati ya hizo pesa, Ksh2.5 bilioni zitaenda katika mishahara na Ksh1.5 bilioni ni zitaenda kwa Bunge la Kaunti ya Machakos na mambo nyingine. Bw. Spika wa Muda, ukifanya hesabu, utagundua kwamba pesa ambazo zimetengewa miradi ya maendeleo katika Kaunti ya Machakos ni Ksh1.4 bilioni na tuna maeneo nane ya uwakilishi bungeni ambayo yanatumika kama kaunti ndogo. Kwa hivyo, Kaunti yangu ina kaunti ndogo nane. Ukigawa pesa hizo, kila kaunti ndogo itapata Ksh150 milioni. Hizo ni pesa ambazo nilikuwa napata kama Mbunge. Hiyo ndiyo pesa inayoenda kwa kila kaunti ndogo ya Kaunti ya Machakos. Ni nini tumebadilisha katika siasa zetu za ugatuzi? Ni jina tu. Ni aibu kwamba tunakalia mikeka miekundu hapa, tunazunguka juu ya hii zuria na wananchi wetu tunaowaongoza kule Pokot wanatembea wakila mbegu za miti. Hiyo ni aibu kubwa. Najua nimeguza nyaya za stima lakini wachazichome zitakaowachoma, maana lazima ukweli udhihirike. Kiasi cha pesa ambazo kaunti ndogo inapata katika Kaunti ya Machakos ni Ksh150 milioni na ni sawa na mshahara wa Mbunge. Kwa nini tutengeneze Seneti, tuwalipe Maseneta na magavana mishahara na kuwanunulia magari kutumia mgao ulikuwepo kabla ya ugatuzi? Huu ni udanganyifu, uhuni na ukora. Mpaka ukweli ujitenge, la sivyo, hakuna mahali tunaenda. Hakuna gavana hata mmoja ambaye anataka kuwaambia watu wake kiasi cha pesa ambazo kaunti yake imepewa na Serikali Kuu katika mgao huu. Kwa mfano, tungetarajia Gavana wa Kaunti ya Machakos kuwaeleza watu wake kuwa kaunti yetu imepatiwa kiasi hiki cha pesa na tutazitumia kwa njia hii ama ile. Wananchi wanaambiwa kwamba bajeti imesomwa, lakini hawaoni mradi wowote ambao unatatekelezwa kutokana na bajeti hiyo. Bw. Spika wa Muda, imekuwa ni mchezo wa paka na panya kwa sababu watu wengine wana pesa ya kuwaajiri mawakili kushughulikia shutuma zingine na pesa za The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}