GET /api/v0.1/hansard/entries/605261/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 605261,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/605261/?format=api",
    "text_counter": 340,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kucheza mpira na karata. Tunajua kwamba kuna washukiwa wengine ambao wakipelekwa kortini wanasema kwamba hawafai kushtakiwa kwa sababu korti imetoa amri kwamba wangojee. Sisi hatutaki kuingilia kazi ya mahakama, lakini tunasema kwamba sheria itumike kwa kila mtu kwa usawa. Nimewasikia wenzetu ambao ni Wabunge wa Bunge la Kitaifa wakikashifu na kutumia matusi ambayo hayakubaliki. Seneti imeitwa majina, tumeitwa watalii na watu wakungoja Ksh1.6 milioni kila mwezi na kila mwaka kama pesa za kutembelea kaunti na kupiga siasa katika mikutano ya hadhara. Bw. Spika wa Muda, Wabunge wanaosema kwamba Seneti haitaki pesa ya kuangalia maendeleo ni wao hao wanaosema kwamba magavana hawafanyi kazi inayofaa lakini wao wanapewa pesa za CDF ambazo wanasimimia. Sisi kama Seneti, tunataka kuonyesha uongozi mwema. Nataka Sen. Kagwe awe na uwezo wa kuungana na Sen. (Dr.) Khalwale, waje kwangu Machakos kuangalia ni maendeleo gani yamefanyika kwa kaunti ndogo na wawasilishe ripoti hapa Bungeni. Maseneta wenzangu; Mheshimiwa Kagwe, Mheshimiwa Khalwale na Mheshimiwa Orengo watawaambia ukweli wa mambo yalivyo kule mashinani. Vile vile, mimi nitatembea kwa kaunti zao nikiwa na wezangu na nitakuja hapa na kuwapa ripoti kamili kama ugatuzi unafanya kazi au la. Badala ya kufanya mambo hayo, Wabunge wanaangalia jinsi watakavyofaidika na kuwatusi Maseneta ambao wanatetea ugatuzi. Bw. Spika wa Muda, kuna mpango wa kuvunja serikali za ugatuzi Serikali ya Jubilee inataka kuvunja Bunge la Seneti. Seneti ikiisha hakutakuwa na ugatuzi katika taifa letu. Magavana ambao hawatakuwa tayari kufanya kazi na Serikali iliyopo watafagiliwa. Tusipotunza ugatuzi na kusimama imara na tuache ukabila tunapotekeleza kazi zetu kwa sababu hii ndio Bunge ambayo ina kiini, maarifa na heshima kuu ya kusimama, kutetea Wakenya na kuwaunganisha, tukiangalia mambo ya Bunge la Kitaifa tunajua kwamba mambo yataharibika. Kwa hivyo, bila kubembelezana na kuangalia nyuma, tunataka kuwaambia Wabunge wa Bunge la Taifa kwamba lazima tujitahidi kuona kwamba zile pesa ambazo zimetengewa miradi ya maeneo Bunge; yaani CDF, zinarudishwa mahali zinafaa kutumika. Hatutaki visa vya gavana kujenga darasa ya mita mbili halafu Mbunge anakuja kesho na Ksh3 milioni na kuongezea futi au nusu mita pale pembeeni kisha anasema kwamba amejenga darasa. Kama gavana anajenga shule, Mbunge naye anafaa kununua viti ambavyo vitatumiwa na wanafunzi katika darasa hilo. Hizi ni pesa za wananchi na si za mtu kuweka katika akiba na kutembea nazo. Tunataka kuona pesa za Serikali zimewekwa katika mahali moja na zitumiwe vizuri Ninataka kuwaambia wenzangu kwamba hatuhitaji kushindana kuhusu nani anajenga hiki ama kile kwa sababu tukitoa pesa hizo wengine watamaliza miaka mitano bila kwenda nyumbani kwa maana wanaenda kujigamba na kusema kwamba wameleta hundi ya kuwasaidia wananchi. Tukitoa jambo hilo, watakuja hapa na kutuuliza kama Seneti tuwaonyeshe njia. Bw. Spika wa Muda, naunga mwenzangu Sen. (Dr.) Khalwale kuhusu mambo ya ukabila katika taifa letu. Mjadala ambao unaendelea kuhusu kumng’oa mamlakani Bw. Tobiko, wale wanaosema hivyo hawasemi mtu wao hatolewi lakini mtu wao akishikwa, wote wanaungana pamoja. Wengine wamesema kwamba Wabunge kutoka mkoa wa kati The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}