GET /api/v0.1/hansard/entries/60540/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 60540,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/60540/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw. Spika, shukrani kwa kunipa nafasi hii ili nitoe usia wangu kuhusu Hotuba iliyotolewa na mhe. Rais kwenye kikao cha jana cha Bunge hili. Nikiitukuza Hotuba hii, kuna jambo moja au mambo mawili nitakayoyazungumzia. Rais alitupa mwongozo kwamba Bunge hili lina jukumu na kazi nzito ya kufanya haswa kupitisha Miswada kadhaa. Alitoa mifano ya Miswada kumi. Unapoiangalia Miswada hiyo, utaona kwamba mingine inarudiana. Miongoni mwa Miswada aliyotaja ni Mswada wa Tume ya Haki za Binadamu na Usawa. Mswada wa nane ni Mswada wa Tume ya Utoaji Haki. Hizo Tume mbili zinazonuiwa kubuniwa kupitia Miswada hii zingewekwa pamoja na kuwa Tume moja ili tuokoe hela ambazo zingetumika kwa minajili ya kazi nyingine nchini badala ya kuajiri watu kwenye Tume ambazo zitakuja kupigania nafasi ya utekelezaji wa kazi hapa na pale. Hata hivyo, tutajua yaliyotendeka na kujua tutaenda wapi. Hatuwezi kujua matokeo kwa sasa. Hivi sasa, tuko chini ya Katiba mpya, ambayo imeratibishwa na nchi hii kwa haraka. Kutakuwa na shida hapa na pale, tukijaribu kuitekeleza Katiba hii kwa mambo kadhaa. Kenya ni nchi katika eneo la Afrika Mashariki, na ilijiunga tangu hapo awali kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki. Hivi sasa, tumeratibisha Katiba mpya, ambayo inasema tutasoma Bajeti yetu katika mwezi wa tatu kila mwaka."
}