GET /api/v0.1/hansard/entries/60543/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 60543,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/60543/?format=api",
    "text_counter": 254,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, kwenye Katiba mpya, tunasema kwamba Kenya inaheshimu mikataba yote ambayo imefanywa na nchi nyingine pamoja nasi. Mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki unasema kwamba mataifa yote wanachama wa Jumuia hiyo yatasoma Bajeti zao wakati mmoja, katika mwezi wa sita kila mwaka. Sisi, Kenya, tumeshaweka kidole na kukubaliana na kipengele hicho. Hivi sasa, mhe. Raila amekuwa akitueleza jinsi tulivyopiga hatua kwenya mambo ya kiuchumi. Tukisoma Bajeti yetu mwezi wa tatu na mataifa mengine wanachama yasome Bajeti zao mwezi wa sita, tutakuwa tumeutupilia mbali Mkataba wa Jumuia ya Umoja wa Afrika Mashariki. Je, itakuwaje? Hilo ni suala ambalo ni lazima lifikiriwe na maafikiano yafikiwe kwa sababu tayari tumevunja Mkataba huo. Hata hivyo, iwapo tutaisoma Bajeti yetu katika mwezi wa tatu na kuwapa nafasi wenzetu kuisoma na kuielewa Bajeti hiyo halafu watoe mapendekezo yao mwezi wa sita, uchumi wetu utaathirika namna gani? Bw. Naibu Spika wa Muda, haya ni baadhi ya mambo ambayo niliyazungumzia wakati baadhi yetu tulipokuwa tukipinga mambo fulani kwenye Katiba hii, lakini Katiba ilipitishwa. Tukasema ni sawa, wengi wape lakini mambo haya yatakuja kutuathiri. Majuto ni mjukuu! Tunaongea mambo ya haki kila siku. Tunapozungumzia uchumi, tunazungumzia haki. Tunapozungumzia polisi, tunazungumzia haki. Je, haki hiyo itatekelezwa jinsi viongozi wanavyosema? Mimi niliathirika katika mwaka wa 2007/2008, kufuatia fujo za kura. Baadhi yetu hapa hawajui maana ya kuathirika kufuatia fujo hizo. Isingekuwa Mungu ananipenda, ningekuwa kule vijijini kama waathiriwa wengine. Watu wengine wanaona kwamba hili ni jambo la mzaha. Mimi nilipoteza mali nyingi, lakini basi sivyo. Jambo ni kwamba, je, haki kwa mnyonge itatendeka? Bw. Naibu Spika wa Muda, kukaja tume ya Kivunja, na nikaathirika; kwa sababu wakati wa mapambano kati ya mirengo ya “Ndiyo” na “La” kwenye kampeini za kura ya maoni kuhusu Katika mpya, nilisema mambo fulani, ambayo yalisabisha mimi kushikwa na kutupwa ndani. Nilikuwa nikijaribu kuutetea mrengo wa “La”, ambayo ni haki yangu ya kikatiba, lakini nilishikwa na kutupwa ndani. Hii ni kwa sababu nilitoa mfano wa kitu ambacho kinaweza kutokea Katiba hii ikipitishwa. Lakini, tangu wakati huo, nimewasikia viongozi, wengine wakiwa majabali wa kisiasa, wakitusi watu na kusema mambo ya fujo kushoto na kulia. Hata wengine walisema kwamba kutakuwa na vita wakati wa uchaguzi wa mwaka wa 2012, eti kama watu sita hawatapelekwa The Hague. “Kivunja wanyonge” amenyamaza. Mimi niligongwa kwa sababu ninatoka kwa jamii ndogo; na hiyo ndiyo inayoitwa “haki”."
}