GET /api/v0.1/hansard/entries/60546/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 60546,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/60546/?format=api",
    "text_counter": 257,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ningefurahi kama Mzee Kibaki katika hotuba ya jana, kidogo angetaja mambo ya wakimbizi wa ndani. Waziri Mkuu amesema hapa kwa uchungu na hatumlaumu kwamba wale walioathirika wanyeshewe na mvua hii ya masika sasa, na hakuna anayejali kuyasema haya ndani ya Bunge. Yanasemwa kidogo kidogo kule vichochoroni. Tunataka tujue ni wangapi walibaki bila kupewa makao. Si hawa wa juzi tu. Hata kwangu katika mwaka wa 1978, Wakuria walifukuzwa kutoka Trans Mara. Hakuna anayejali maslahi yao katika Serikali yetu. Je, sisi viongozi ambao tumepata nafasi kuwa katika Bunge hili, tutayarekebisha vipi makosa haya? Tunaposhughulikia suala la kuratibisha katiba ya Kenya kwa kuangalia Miswada zaidi ya 25--- Tunatakikana tupitishe kama Miswada 10 ili kuje kabla ya kuwa na uchaguzi. Tunaambiwa kwamba uchaguzi utafanyika chini ya miaka miwili ijayo. Wamesema kuwa uchaguzi ujao utafanyika kama uliwekwa katika Katiba mpya. Walisahau kwamba bajeti ya Kenya inasomawa mwezi wa sita. Je, iwapo bajeti ya mwaka huu na ya mwaka wa kesho haitakuwa mwezi wa sita kwa sababu itakuwa transition, itakuwaje kwamba bajeti isomwe wakati sisi tuko likizoni, au isomwe na hakuna Mbunge wa kuirekesbisha ili Serikali iwe na hela za matumizi? Sisi tunapitisha Miswada tu bila kufikiria mambo fulani. Lakini hatuwezi kufikiria kwa sababu tumeweka vichwa kwa mchanga kama nungu. Lisemwalo lipo, na kama halipo laja. Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda."
}