GET /api/v0.1/hansard/entries/605651/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 605651,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/605651/?format=api",
"text_counter": 57,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Khaniri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 171,
"legal_name": "George Munyasa Khaniri",
"slug": "george-khaniri"
},
"content": "Asante Sana, Bw. Spika. Kwanza kabisa natoa shukurani kwa mzalendo huyu kutoka Mandera ambaye ameweza kuangazia mambo ambayo yanafanyika kule Mandera, yasioambatana na sheria za Kenya. Ningependa kuwahimiza Wakenya wengine wawe macho na kuchunguza kwamba pesa tunazotuma kwa serikali za kaunti zinafanya kazi ambayo zilipangangiwa, ikiwa ni majukumu ambayo yamepeanwa kwa serikali hizo za kaunti. Visa vya magavana kutumia pesa tunazopitisha kufanya shughuli ambazo ni za Serikali Kuu ni vingi sana. Si ajabu kupata Gavana wa Mandera na serikali yake wakitumia pesa nyingi kujenga uwanja wa ndege na barabara ambazo zinafaa kujengwa na Serikali kuu, ilhali shughuli ambazo ni za serikali ya kaunti zinaendelea kugandamizwa."
}