GET /api/v0.1/hansard/entries/605811/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 605811,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/605811/?format=api",
"text_counter": 217,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mositet",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 608,
"legal_name": "Peter Korinko Mositet",
"slug": "peter-korinko-mositet"
},
"content": "Asante sana, Bi Spika wa Muda, kwa kuniruhusu nichangie huu Mswada. Ni furaha kwetu sisi Maseneta kwa sababu tunajua kwamba jukumu kubwa tulilopewa na wananchi walipotupigia kura ni kuhakikisha tumepigania pesa zaidi ziende kule mashinani kama vile Katiba inasema. Kama vile Mwenyekiti wetu, Sen. Billow, alivyosema, kweli safari ya kutafuta hizi pesa ilikuwa ngumu sana. Ni kama ile ya Musa ambapo ilimbidi apasue jiwe ndipo maji yakatoka. Ni kero sana kwetu na kwa wananchi hasa tukishajua pesa ambazo ni ngumu kupata zitatumika kwa njia mbaya. Kaunti yangu ya Kajiado imepewa pesa zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita. Mwaka huu wa 2015/2016 watakuwa na Kshs4.4 bilioni. Itakuwa furaha yangu napia wananchi wa kaunti hiyo kuona zile pesa zimetumika vizuri ili kupunguza shida zinazowakumba. Ikiwezekena, viongozi wa daraja zote tushirikiane kabisa kupunguza hizi shida. Haifai watu kuanza kufikiria vile hizo pesa zitaendakwa mifukoni ya watu wengine."
}