GET /api/v0.1/hansard/entries/605814/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 605814,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/605814/?format=api",
    "text_counter": 220,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bi Spika Wa Muda, ninapongeza Kamati hii kwa kufanya kazi nzuri kabisa. Imejitokeza waziwazi kwamba sio lazima Seneti iwe pamoja na IntergovernmentalBudget and Economic Council (IBEC). Wacha timu ya IBEC wafanye mikutano yao, washauriane na waseme ni pesa ngapi zitaenda kwa kaunti. Dakika ya mwisho, walio na nguvu na uwezo wa kusema ni kiasi gani kitafika huko ni Seneti. Wenzetu tunaowapenda na ambao pia walipigiwa kura kama sisi, waliona tulichofanya na wakasikia uchungu. Hata hivyo, hizi pesa zinaenda mashinani. Katiba inawapa nguvu na uwezo wa kuangalia jinsi zile pesa zinatumika kule mashinani.Kwa hivyo, tushirikiane tuone kwamba hizi pesa zinatumika kumaliza shida za wananchi. Tuone kwamba hospitali zina madawa na barabara zimetengenezwa. Bi Spika wa Muda, safari ilikuwa ndefu lakini sasa tunaona tumefika kikomo chake. Hata kama tunahisi kwamba pesa hazitoshi, aghalabu ni vizuri kuna pesa zinazoenda katika kaunti zetu. Hii ndio furaha yetu. Ni jukumu la MCAs kutusaidia kufuatilia ili kuhakikisha kwamba matakwa ya wananchi yanatimizwa. Pesa ambazo wananchi walisema wangependa zitengeneze barabara, hospitali na shule za chekechea, waone kwamba zimetumika kwa shughuli hizo bila kupelekwa kwingine. Wachunguze iwapo wanapata thamani ya pesa zilizotengewa miradi kadha wa kadha. Isije ikawa mradi unasemekana ni wa Kshs5milioni,ili hali ni mradi ambao ungefanywa na kiasi cha Kshs1 milioni moja. Tunajua wana uwezo wa kufanya hivyo na pahali ambapo wanahisi hawana uwezo, basi waombe usaidizi wa Seneti. Ingawa tumepokonywa pesa ambazo tulifikiria tungetumia kukagua miradi na kuhakikisha ufisadi hautafanywa katika kaunti zetu, tutaendelea kuhakikisha pesa hizi zimetumika vizur. Ninaomba Maseneta wenzangu, tusichoke kuomba kama jinsi mapadre wanavyofanya. Mimi ni Mkristo na ninajua wachungaji wengi huomba kabisa.Wakipata walichoomba wao hufikishia waumini wao. Nasi tuendelee na hilo jukumu letu. Bi Spika wa Muda, kuna Wizara ambazo zinahusika kwa utoaji wa misaada ya kusaidia katika miradi ya maji, afya na kadhalika. Ningeomba Wizara hizo kuwahusisha Maseneta ili wajue kwamba kuna wahifadhi ambao wangependa kuanzisha miradi fulani katika kaunti zao. Tukifanya hivyo, miradi yetu itafanywa kwa njia ya utaratibu. Bi Spika wa Muda, baadhi ya kaunti zetu zina changamoto nyingi zinazoambatana na ufugaji. Kwa mfano, kuna magonjwa ya mifugo, hasa wakati huu wa masika ambao kumekuwa na mvua nyingi. Ni vizuri magavana na serikali zao watafute namna na kuhakikisha kwamba mifugo, hasa ng’ombe zinachanjwa vizuri na kutafutiwa madawa yanayofaa. Hatutaki kuona wanyama wetu wakifa kwa sababu ya magonjwa mbalimbali. Ninawasihi magavana kutoka kaskazini mwa Bonde la Ufa, wahakikishe kwamba wametenga pesa katika bajeti zao kusaidia kilimo. Tunajua kwamba mkaguzi mkuu wa pesa za Serikali hana uwezo wa kufanya ukaguzi katika kaunti zote. Hata hivyo, ninamsihi ajaribu kufuatilia pesa ambazo zitapelekwa mashinani na kuhakikisha zimetumika vizuri. Inafaa wajiotelee kama wazalendo na wafanye kazi yao kama inavyohitajika. Hatutaki kuwaona wakiwa na vikapu vya kubembea pesa hizo ili wasionyeshe maovu katika kaunti zetu. Inafaa wajue"
}