GET /api/v0.1/hansard/entries/605817/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 605817,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/605817/?format=api",
    "text_counter": 223,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kwamba hizi pesa ni za wananchi. Uchunguzi wake utaonyesha kama pesa hizi zimetumika vizuri au kuna ufisadi fulani. Hata magavana wakipiga kelele, mwishowe ni yeye atakayekagua na kutueleza vile pesa hizo zimetumika. Bi Spika wa Muda, ufisadi ndio ugonjwa mkubwa kabisa katika Taifa la Kenya. Tuna Katiba nzuri ambayo inaweza kutupeleka mbele na ambayo ni tegemeo la Kenya miaka za usoni. Lakini itakuwa tofauti kabisa ikiwa tutapigana na ufisadi na kuumaliza. Ningependa kuwaeleza viongozi wote, hasa ndugu zetu ambao wako katika Bunge la Kitaifa kwamba inafaa wajitahadhari ndivyo tuweze kuangamiza ufisadi. Inafaa ofisi kama ile ya mkakuguzi mkuu wa pesa za Serikali ipewe ufadhili wa kutosha. Itakuwa jambo la aibu kusema kwamba tunapigana na ufisadi ilhali ile ofisi ambayo ingetusaidia haipewi pesa za kutosha. Hivyo ni kusema kwamba wale wanaonyima hiyo ofisi ufadhili, wanataka ufisadi uendelee mbele. Lakini ikiwa tunawafadhili vilivyo na hawafanyi kazi yao, basi inafaa waondolewe mara moja kutoka ofisi hizo. Inafaa sisi sote kama Maseneta kuhakikisha pesa hizi zimetumika vizuri. Ingwa tumenyimwa pesa za kufanya kazi hiyo, ni lazima tuendelee na kazi yetu. Tumekuwa tukifanya hivyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na tutaendelea. Bi Spika wa Muda, kwa hayo machache, niinaunga mkono."
}