GET /api/v0.1/hansard/entries/606281/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 606281,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/606281/?format=api",
    "text_counter": 109,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Njoroge",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13158,
        "legal_name": "Ben Njoroge",
        "slug": "ben-njoroge"
    },
    "content": "Ni kutokana na mahitaji ya Katiba ambapo tuliteuliwe kutoka vyama tofauti ili kuwakilisha baadhi ya watu kama vile walemavu, vijana na akina mama. Sisi pia tuna majukumu ambayo tunahitajika kutekeleza kule mashinani. Tulikuwa tumeona mwanga kwamba tutaweza kufikia wale ambao tulikuja kuwakilisha kule mashinani ili tuweze kuangalia jinsi wanavyohudumiwa endapo tungetengewa fedha. Hata hivyo, ndoto hizo zilitupiliwa mbali na Bunge la Taifa. Bunge la Taifa lilitupilia mbali matarajio yetu na kuona kuwa hatufai kabisa, kama Seneti, kuenda kule mashinani ili kuokoa uporaji wa fedha za wananchi wanaolipa kodi ambao umekuwa ukiendelea. Kwa hivyo, kamati inayotarajiwa kuundwa katika Seneti hii ni kamati ambayo imekuja wakati unaofaa hata kama imechelewa. Ni vizuri tuchukue mwelekeo ambao utaeleweka. Kama alivyosema Seneta mwanzangu hapa, tunasema kitu kimoja kila siku kunapotokea mvurutano kama huu. Ni vizuri turejelee Katiba, tuifungue na kuiangalia ili The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}