GET /api/v0.1/hansard/entries/606285/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 606285,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/606285/?format=api",
"text_counter": 113,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "inayohusisha Bunge la Taifa na Seneti ili Seneti iweze kujisimamia kwa sababu Bunge la Taifa halina heshima hata kidogo. Sijui linafuata Katiba gani. Madharau ambayo Wabunge wa Bunge la Taifa wameonyesha kwa Bunge la Seneti ni jambo la kusikitisha sana. Ikiwa tutaendelea kushirikiana pamoja katika PSC, hii Seneti haitasonga popote. Hii itawafanya waseme kuwa haina haja kuwa na Seneti katika nchi hii. Kwa hivyo, Bi. Spika wa Muda, maoni yangu ni kwamba wakati umefika sasa. Ukisukumwa kwa ukuta mara nyingine, inabidi uanze kupigana ukielekea upande wa mbele. Hakuna lingine ila kurejelea Katiba na kuangalia vipengele ambavyo vinafaa kubadilishwa. Ni lazima vipengele vinavyofaa kubadilishwa vipelekwe kwa wananchi ili viweze kubadilishwa kulingana na vile Katiba yenyewe inasema. Wakati umewadia ambapo Rais na Naibu wake wanafaa kufikiria mara mbili wanaposhauriwa na washauri wao kuhusiana na mambo ya kisheria. Hii ni kwa sababu ni mara nyingi sana tumeona Rais akipewa ushauri ambao hauambatani na vile Katiba inavyosema. Mara nyingi amepitisha mambo ambayo ni kinyume na vile Katiba inavyosema. Kwa hivyo, ni vibaya sana Rais kukaa na watu wanaoitwa sycophants ; watu ambao wanamwambia kile ambacho wanasikia lakini wanakosa kumwaambia ukweli kwa sababu ukweli lazima uambatane na vile Katiba inavyosema. Kulingana na wajibu ulionileta katika hii Seneti na kazi ambayo nimepewa katika Kipengele cha 96 kwenye Katiba, inaonyesha wazi ya kwamba kama Rais mwenyewe hatakuwa mwangalifu – kupitia kwa wale wanaomshauri – itakuwa vigumu sana yeye mwenyewe kutekeleza majukumu yake na kuiacha Seneti ifanye kazi yake kulingana na vile Katiba inavyosema. Nimesema hayo na ninataka kueleza kwa sababu mara nyingi watu hukimbia kwenda kumwambia Rais kwamba Sen. Njoroge alikuwa anasema hivi. Nasema wazi nikiwa hapa mbele ya Bunge hili. Ni lazima Rais mwenyewe pamoja na Naibu wake wajiepushe na watu wanaowapotosha kwa sababu sisi sote tulitumika katika kuomba kura na kuwaingiza katika nyadhifa mbalimbali, haswa watu kutoka mrengo ambao mimi niko. Sikutarajia ya kwamba wakati kama huu utafika. Hii ni kwa sababu nilipopewa wadhifa huu haswa na chama ambacho kinatawala, nilifikiria ya kwamba tufanye kazi kulingana na vile Katiba inavyosema. Hata hivyo, naunga mkono kwamba kamati inayotakiwa kuundwa iundwe. Asante sana, Bi. Spika wa Muda."
}