GET /api/v0.1/hansard/entries/606311/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 606311,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/606311/?format=api",
"text_counter": 139,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kama walisema Seneti isije ikafanya chochote tena, lakini nataka kupongeza Seneti kwa sababu ilionyesha uhodari na ukweli kwamba serikali za kaunti zinahitaji pesa kwa sababu ya hospitali na shida nyingi ambazo ziko huko na angalau hiyo Ksh3 billioni zilipatikana zitaenda kwa kaunti zetu. Bi. Spika wa Muda, Katiba yetu ni nzuri sana na inaweza kuendesha Kenya iende mbele kabisa ili tufikie mataifa ambayo yako mbele kimaendeleo. Ugonjwa wetu mkubwa ni ufisadi. Nikiangalie vile Bunge la Kitaifa lilifanya kwa kupunguza kiwango cha pesa kwa asasi mbali mbali za Serikali na Seneti, hii ni kusema kwamba Wabunge wa Kitaifa wanataka ufisadi uendelee. Kwa nini nasema hivyo? Huu mtambo wa IFMIS ambapo tunasema kaunti zote ziunganishwe na kauti ndiyo malipo ya pesa yawe tu ya kupitia kwa makaratasi ili tumalize ufisadi. Ili bunge za kaunti ziweze kujisimamia na kutumiwa pesa bila kupitia kwa magavana ambao wanaweza kutumia pesa hizo kwa miradi mingine, lakini Bunge la Kitaifa lilipunguza pesa hizo ili ule mtambo usiweze kufikia wale. Jambo lingine ni kuhusu korti zetu ambazo tunatumia kwa wavunja sheria ambao wamenaswa kama kuiba mali ya umma lakini pesa zao zilipunguzwa. Hii ni kuhimiza ufisadi. Itakuw shida kubwa kwa Maseneta e ambao kwa miaka miwili wamejaribu kupigana na ufisadi kule mashinani kwa sababu wanahitaji nguvu ili waweze kufika pale. Hiyo nguvu ilikuwa ile Kshs1 billioni lakini ambayo iliondolewa na Bunge la Kitaifa. Ni nani atalinda na kutetea matumizi ya Kshs290 bilioni ambazo zimetumwa kule mashinani? Hiyo ni kama kusema ufisadi uendelee. Taifa limefika mahali ambapo maombi yanatakikana. Tarehe 28 tulikuwa na maombi ya kitaifa na baada ya hiyo, ile hekima tuliona Wabunge wa kitaifa wamepewa ni ile walienda kutenda pale. Juzi, tuliona vile walimtendea Dkt. Juma. Aliambiwa kuwa ana shahada na ujuzi wote lakini kwa sababu aliwakataza Wabunge kufika kwa ofisi yake, na sio Wabunge tu wa kitaifa pia Wabunge wa Seneti, ilikuwa ni shida. Sisi kama Bunge la Seneti hatujapiga kelele, hatujasikia Mbunge yeyote wa Seneti akisema kwamba kwenda kwa Dkt. Juma ni makosa, ama ile barua ambayo iliandikwa tukaona yale waliyoyapata. Mimi kama mmoja anayemwamini Mungu sana, wale ndugu zetu sijui ni wingi unaowasumbua na kama ni wingi unawasumbua, ningeomba wakati Miswada ambayo inaguza taifa nzima kupelekwa na kwenda kushambuliwa kwa njia ambayo haifai, na ambayo haina hekima kwa wale viongozi ambao wananchi waliwapigia kura wakijua watalichukua taifa na kulipeleka mbele, imefika mahali na tuseme kwamba roho mtakatifu aweze kurudi kwao. Watafute maombi mengine kama ni Wakristu wapakwe mafuta na kama ni Waislamu waende kuhiji ndio wakirudi waweze kupata hekima. Nasema hivi kwa sababu hekima ni kitu cha maana kwa kiongozi. Kiongozi anayependa taifa lake ni yule anajishusha kama vile Seneti haikuona inahitaji zaidi ya Kshs1billion au malumbano ya hiki na kile. Tuliona tukijishusha chini mwaka wa 2013/2014, 2014/2015 na hata wakati huu bado tunajishusha, wale pia wanafaa kujishusha ili tuweze kuhudumia taifa hili kwa njia inayofaa. Bi. Spika wa Muda, kama nikuonyeshana nguvu za kila mmoja basi taifa hili haliwezi likasonga mbele. Sisi sote tumeenda shule na vyuo vikuu na tunajua tuna waalimu ambao wanasomesha pale, na wana uwezo wa kuangalia mitihani ili tuweze The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}