GET /api/v0.1/hansard/entries/606313/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 606313,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/606313/?format=api",
"text_counter": 141,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kupita, hatujawahi kusikia siku moja kwamba wanatumia nguvu zao kuwakataza watu haki zao. Ningeomba baadhi ya Wabunge, kwa maana sio wote lakini kuna wengi wao - Sijui ni wingi wao kwa sababu wako 290 inawasumbua? Heri kabla Hoja hizo kupelekwa, waweze kuziangalia na kuzipitisha, wawe wanapata nafasi katika vikao vya Kamukunji na wawasikilize wataalamu ili waweze kuelewa Hoja ambayo iko mbele yao, ili wasije wakachukua ule mwenendo kwamba wamesema jambo bila kulifuatilia.Ukikuta watu wanakimbia na wewe unakimbia bila kuelewa wanakimbia kwa sababu gani, baadaye ndio unasema mimi ndiye ningesaidia hii na kwa nini ilifanyika halafu hasara inaingilia taifa. Hii inafanya wananchi wetu kujiuliza walichagua viongozi wa aina gani. Hekima iliwapotea ikaenda wapi na kila Jumapili tuko kanisani? Tofauti yetu na Wabunge wa kitaifa ni kwamba mimi kama Seneta ninataka pesa ziende kwa Kauti ya Kajiado, na ningeulizwa ningesema ziwe nyingi kabisa. Seneta Wetanguala wa Bungoma pia anataka vile vile. Kwa hivyo, tunakubaliana pesa ziende kule mashinani, lakini wale wanataka mradi wa kwao tu. Mimi najiuliza ndio ili taifa liwe taifa, viongozi walipigana na Uhuru ukapatikana. Ndio tupate ukombozi wa katiba wengine walifanya vile vile. Katika taifa ili ugonjwa mkubwa ni ufisadi. Mambo mengi yamesemwa kuhusu Wabunge wa Kitaifa na bado wanaendelea na ule mwenendo. Jameni, walio na hekima katika Bunge lili, tafadhali wasimame na wengine na waonyeshe njia kwa sababu tumepotea na tunapaswa kwenda kwa ile njia ambayo hekima inatuonyesha ya kwamba taifa ili litainuka tukifanya hili. Bi. Spika wa Muda, nikichangia upande wa Bajeti ambayo ilipitia hapa, kweli kabisa tuliona hakuna pesa zingine ambazo zinahitajika kupelekwa kwa kaunti. Pesa za unyunyizaji mimea maji ni shughuli ya kaunti. Zile pesa zingefaa kwa kila kaunti. Zikienda pale, ni wachache watakaopata. Kama kila kaunti ingepata, wangehakikisha usawa upo kwa vile kila wodi ingekuza mimmea. Tuangalie pesa zilizotengewa NYS. Ninavyozungumza sasa, lori zao zinachukua mawe kutoka Kaunti yangu, zinapitia upande wa Ongata Rongai na zimeharibu barabara. Hata wakiambiwa wamwage mawe lori tano katika hiyo barabara wanayopitia ndio aghalabu iwe sawa, hawajali. Barabara nyingine inayotumika ni ile inayotoka Kitengela hadi Ongata Rongai ilhali kaunti yangu hailipwi hata ndururu. Bi. Spika wa Muda, mimi ninaonelea umefika wakati Wabunge wa Bunge la Kitaifa wajaribu kuangalia usawa na ugawaji wa pesa uko namna gani. Hata kama ni CDF, Katiba ni wazi na hatufai kujidanganya kwa kusema kuwa tunaweza kuieweka Katiba kando. Katiba inasema wazi wazi pesa ziwe kwa kaunti na pia katika Serikali ya kitaifa. Iwapo wanataka kurekebisha CDF Act ndipo miradi iwe ya kitaifa hasa ya upande wa elimu, pesa hizo basi ziende kwa Prof. Kaimenyi. Hakuna njia nyingine. Ule Mswada lazima upitie kwenye Seneti na itakapofanya hivyo, hekima itupate na tuhakikishe kwamba pesa hizo zimetumika vizuri. Ninaunga mkono."
}