GET /api/v0.1/hansard/entries/60791/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 60791,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/60791/?format=api",
    "text_counter": 167,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwahima",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 99,
        "legal_name": "Mwalimu Masoud Mwahima",
        "slug": "mwalimu-mwahima"
    },
    "content": "Ningependa kuomba kwamba, sisi, Wabunge ambao tumechaguliwa kutoka sehemu mbalimbali, tushikane tufanye kazi pamoja tukijua kwamba wakati wa uchaguzi utakapofika tunaweza kurudi Bungeni ama tusirudi, lakini tuhakikishe kwamba tumeiweka Kenya vizuri. Hivi majuzi, tulikuwa na shida ya uteuzi wa maafisa wakuu wa umma. Tukavutana mpaka sasa tumefikia mahali ambapo shughuli hiyo inaendelea vizuri. Bw. Naibu wa Spika, langu ni kusisitiza kwamba sisi, tukiwa Wabunge, tufanye kazi na watu vizuri ili tuweze kuwa na Serikali nzuri. Itakuwa aibu kubwa kwetu sisi viongozi tuliochaguliwa kama tutashindwa na uongozi, kama kwingineko Barani Afrika. Viongozi kule Misri wameshindwa na uongozi licha ya kwamba wao siyo makabila mengi. Sisi tuko makabila 42 lakini tumeweza kusikizana na tunaishi vizuri."
}