GET /api/v0.1/hansard/entries/608015/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 608015,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/608015/?format=api",
"text_counter": 200,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Pia mimi nataka kujiunga na ndugu zangu, Maseneta kumpatia heko Sen. (Prof.) Lonyangapuo kwa kuleta Mswada huu. Jambo la kwanza, ningetaka sheria hii ichukue mkondo kila mahali katika nchi hii. Hili likifanyika mimi, kama mkaazi wa Kilifi, nina imani kwamba hawa KPRs wataweza kutekeleza amani pale ambapo askari wetu wa kawaida huwa wanazembea. Hivi majuzi, tumempoteza askari wetu mmoja huko Kaloleni kwa sababu ya upungufu wa maaskari. Kwa hivyo, tukiwapata maaskari wa KPR, huenda ikawa jambo nzuri zaidi. Bw. Naibu Spika, natumai kwamba hakutakuwa na ubaguzi katika wale watakaochukuliwa kama maaskari wa KPRs ili wale watu wanaotoka katika eneo lile wapewe nafasi hiyo. Si polisi wote ambao ni wabaya, hasa kule Kilifi."
}