GET /api/v0.1/hansard/entries/608162/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 608162,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/608162/?format=api",
    "text_counter": 347,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "I hope my time is checked. Bw. Spika wa Muda, tunaona ya kwamba wanaofaidika katika mmea wa viazi hasa ni wakulima. Nilipokuwa Mwenyekiti wa Shirika kuu la Agricultural Society of Kenya (ASK), tuliona ya kwamba wakulima hawapewi kipaumbele. Wakulima wanawekwa nyuma kwa sababu hawapewi nafasi ya kuona ya kwamba mimea yao imewapatia faida. Kitu ambacho kinatutia moyo zaidi ni kwamba mmea wa viazi pia umeweza kufaidisha wanabiashara na kuondoa umaskini. Kwa hivyo, huu ni mmea ambao Serikali inastahili kuutilia kipaumbele. Huko Pwani, kuna mmea wa korosho ambao umetuondolea umaskini. Hii ni kwa sababu miaka miwili au mitatu baada ya kuupanda mmea huu, wakulima wamepata faida tele. Mmea huu umeweza kuwasomeshea watoto na mimi mwenyewe ni kielelezo; nilisomeshwa kutokana mapato kutoka kwa korosho. Nakumbuka zaidi, tulipokuwa vijana huko Pwani, Kaunti ya Kilifi pamoja na ya Kwale ndizo ziko na mimea ya korosho. Huu ndio mkadirio wa wakulima wa Pwani. Mmea huu umetuletea faida ya kifedha na kuimarisha uchumi wetu. Ukiangalia maisha ya watu wa Kaunti ya Kilifi, wakati mmea huo ulikuwa unapandwa na kuleta faida, watu wa Kilifi waliboreshea uchumi wao katika miaka ya 1960 na 1970. Lakini la kusikitisha, Bw. Spika wa Muda, ni kwamba katika miaka ya mwisho wa 1980, kuingilia 1990, mabwenyenye wengi waliingilia kiwanda cha korosho na kuiba mali na kuona kwamba mtambo huu hautalipa ridhaa za wale wakulima waliopeleka korosho zao kwenye kiwanda hicho ili wapate faida na kusomesha watoto wao. Ni jambo la kusikitisha ya kwamba hakuna hata hatua moja iliyochukuliwa kwa mabwenyenye hawa kuwashtaki. Hawa ni wakenya, wakurugenzi wa Kenya CashewnutCompany Limited (KCCL) ambayo ilikuwa huko kilifi, waliochukua pesa, wengine walichukua mikopo kutoka kwa benki lakini pesa hizo hazikuregeshwa. Hatimaye waliweza kukibwaga kiwanda hicho. Serikali lazima ichukue hatua kuona kwamba wale walioangusha KCCL wameshikwa na kuulizwa ni kwa sababu gani walifanya makosa kama hayo na hatimaye washtakiwe kortini. Ikiwa itawezekana mali yao yote ambayo walikuwa nayo iregeshwe. Tuko na vipengele vinavyosema kwamba kama ulichukua mali ya haramu utaregesha. Kwa hivyo, wale ambao walipata mali kupitia kiwanda hicho na hatimaye wakakiua wachukuliwe hatua. Sisi tunasema kwamba katika hizi serikali zetu zilizokuwako, hasa serikali yetu ya pili, hii ni serikali ambayo ilikuwa imeruhusu watu hao watende kitendo kama hicho. Tuliweza kuuliza serikali ya tatu ya kwamba waregeshe kiwanda hicho na wakasema wataregesha lakini hatimaye haikuwezekana. Hivi sasa tunajua serikali iliyoko ni serikali ya Jubilee na inajua historia hii yote. Lazima hatua ichukuliwe sasa na tunataka Serikali hii kuhakikisha kwamba kiwanda hicho kimeregeshwa kwa wananchi. Hivi sasa walioko ni watu wanaofanya biashara ndogo ndogo ambao wameondoa mtambo na kila kitu kilichobaki pale ni gofu tu ama sinema, hakuna chochote kinachoendelea kwenye mtambo. Sisi tunasema ya kwamba, Serikali ina uwezo wa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}