GET /api/v0.1/hansard/entries/60831/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 60831,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/60831/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Ninakushukuru Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii. Nanajua tunapochangia Hoja hii ya kwenda likizo, wananchi katika Taifa nzima wametega masikio katika vyombo vya habari kusikia tunagusia nini. Ningependa kugusia wakimbizi wa kisiasa katika nchi yetu, ama wale tunawaita IDPs. Tunapofunga safari na kwenda nyumbani; tumeamka kwenye nyumba zetu na tutaenda katika nyumba zetu. Lakini kuna Wakenya, ambao ni akina mama, watoto na wanaume, walio katika barabara; wanalala katika viwanja. Swali ninalogusia mimi mwenyewe kila mara ninapotembea, na ninaposikiliza vyombo vya habari, ninasikia kwamba kuna Wakenya ambao wanataabika; ninasimama na kujiuliza swali, je tuko Kenya huru ama Kenya ya kikoloni? Nchi ambayo ina uhuru na inajitawala haiwezi kuangalia kwa miaka minne ipite, na wananchi wa taifa hilo hawana chakula, makao na pahali pa kulala. Chanzo cha mambo haya si kuwa hao watu ni masikini. Wengi wao waliuza mashamba yao na kwenda kununua mashamba mengine. Wengine wamefanya kazi miaka nenda, miaka rudi, wakaweka pesa zao kwa miaka 50, 40 au 30, baadaye wakanunua mashamba, lakini siku moja walijikuta wakilala barabarani. Mimi ninatoa mwito kutoka ofisi kubwa katika nchi hii kusema ya kwamba hii ni laana kwa nchi. Hakuna usawa na haki. Kama viongozi tunapotembea, hatuna heshima kwa wale tunaowaongoza. Kwa hivyo, kwa haraka iwezekanazwo kabla ya mwezi wa sita kama vile tulivyoahidiwa, tunataka kuona hawa akina mama ambao wana haki sawa na Rais huku watoto wakiwa na haki sawa na Waziri. Wote hawa wana haki ya kuona kwamba heshima yao imehifadhiwa. Hatutakuwa na amani ikiwa hawa watu wataendelea kuishi barabarani."
}