GET /api/v0.1/hansard/entries/60835/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 60835,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/60835/?format=api",
"text_counter": 211,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Mambo ya magendo na ulaji rushwa yametajwa hapa. Ukiangalia katika mgao wetu wa Serikali, walioko katika PNU hawataki kutaja magendo yaliyoko upande wao na vile vile walioko katika ODM wanajitetea kivyao. Kwa hivyo, tuwache mambo ya kujivuna hapa. Kama ni uwazi wa kupigana na kasumba ya rushwa, isiwe ni mambo ya baba na mtoto na dada na kabila la mtu. Inafaa kila mhusika abebe mzigo wake mwenyewe, aende mahakamani na kushtakiwa. Haifai kuongea juu ya ufisadi mmoja tu kama ule wa hoteli ya Grand Regency. Je mahindi yetu yalienda wapi? Tunajua ni pesa ngapi nchi hii imepoteza na walioiba wanatumia hio pesa."
}