GET /api/v0.1/hansard/entries/60897/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 60897,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/60897/?format=api",
    "text_counter": 273,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Yakub",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 378,
        "legal_name": "Sheikh Yakub Muhammad Dor",
        "slug": "sheikh-dor"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii ambayo ninaunga mkono. Kwanza, ningependa Serikali iwakumbuke Wakenya 13 ambao walipelekwa nchi jirani ya Uganda. Huu ni mwaka wa pili na niliuliza swali kuhusu Wakenya hao13 ambao wako katika Kampala lakini ninasikitika kwamba Wizara mbali mbali zilinijibu kwa barua kwamba si Wizara zao zinazohusika. Hata Mkuu wa Sheria alinijibu kwa barua kwamba jambo hili haliko mikononi mwake. Tungependa Serikali ichukue hatua haraka ili iwarejesha Wakenya hao 13 ambao hawana makosa yoyote nchini Kenya. Bw. Naibu Spika, ninataka kuongea juu ya maswala ya Bandari ya Mombasa. Serikali haikufuata kanuni zilizowekwa kama kuwahusisha wafanyikazi wa bandari, viongozi na washikadau wa Pwani kwenye maswala ya kuibinafsisha bandari. Tunataka Serikali iondoe kwa haraka Kenya Gazette No.70 ya 2009, na kuwe na mpango mpya wa kubinafsisha Bandari ya Mombasa."
}