GET /api/v0.1/hansard/entries/60965/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 60965,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/60965/?format=api",
    "text_counter": 57,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, inagadhabisha na kufedhehesha kwamba wanaopinga mapambo ya mhe. Mbuvi ni wale waliounga Katiba hii mkono. Haya ni baadhi ya manufaa ya Katiba ya sasa ambayo walipigia debe usiku na mchana. Katiba hiyo inasema wazi kwamba kama una itikadi au wewe ni wa dini Fulani, unaweza kuruhusiwa kuvaa kulingana na dini au itikadi hiyo. Vile vile, mhe. Mbuvi ana jina lake la kisasa la utani. Yeye anaitwa “Sonko.” Tabia na mienendo ya akina “Sonko” ndio hii. Sasa anathibitisha wazi kwamba yeye ndio “Sonko.” “Sonko” ni mtu ambaye amerembeka na anavalia vipuli na suti ambayo imenyooka. Kwa hivyo, yote mengine ni maneno tu. Naomba biashara ya Bunge iendelee. Yeye yuko taratibu na Sheria."
}