GET /api/v0.1/hansard/entries/609965/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 609965,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/609965/?format=api",
"text_counter": 117,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "katika Kenya. Lakini hivi sasa ijapokuwa pesa hizi zitapelekwa katika kaunti, watu fulani, haswa Seneti hii, wameadhibiwa kwa sababu ya kuchangia katika kupitishwa kwa pesa hizo. Ugawaji wa pesa hizi si makosa. Tulisema pesa hizi ziende mashinani ili ziweze kuinua hali ya hospitali zetu. Hasa katika Kaunti ya Kilifi hatuna hospitali ya Level 5. Kwa hivyo, tulipitisha pesa hizi ziende kule ili zisaidie kuinua hali ya hospitali ili akina mama wetu wanaotoka pande mbalimbali wapate matibabu mema. Lakini hivi, sasa uamuzi wetu umeleta tetesi. Juzi, nilikuwa katika hospitali ya Mariakani na niliona jambo la kusikitisha. Kuna mama ambaye alikuwa na mtoto mgongoni. Kule kwetu huwa tunatumia majembe madogo madogo kulima. Wakati alikuwa akilima mahali ambapo kulikuwa na nyasi, hakujua kuwa kule ndani kulikuwa na shimo. Hatimaye alipokuwa akishika zile nyasi aliumwa na nyoka. Baada ya kuumwa na nyoka alihisi kama mwili wake wote haumfai. Kwa bahati nzuri mama mkwe alimkimbiza hospitalini ambayo haiko mbali na shamba lao. Baada ya kufika Mariakani alipata matibabu na hali yake ikawa nafuu. Lakini wakati huo mkono ambao uliumwa ulikuwa tayari umegeuka na kuwa rangi nyeusi. Ripoti inayonifikia hivi sasa ni kwamba aliupoteza mkono ule. Hii inamaanisha kwamba pesa hizi zingewasaidia akina mama kama wale. Pia, zitawasaidia akina mama, watoto na Wakenya wote kwa jumla. Hii ndio maana Seneti imesema kwamba pesa lazima ziende kule mashinani. Waswahili kusema kwamba heshima si utumwa. Sisi tunahitaji heshima kutoka kwa wenzetu ambao ni Wabunge. Jambo ambalo nataka kulitia mkazo zaidi ni: Je, korti zetu za Kenya zilifanya makosa gani? Sheria katika Katiba inasema kwamba hauwezi kumpata na hatia hakimu ama jaji kwa uamuzi alioufanya kulingana na kesi iliyo mbele yake. Seneti ilienda mahakamani na kudai kwamba sheria ilikuwa haizingatiwi. Mahakama iliamua kwamba Seneti ilikuwa inasema ukweli. Kwa hivyo, Seneti na mahakama hazikufanya makosa. Lakini Wabunge walichukua hatua ya kuvunja sheria kwa kuadhibu mahakama kwa kuondoa Kshs800 milioni katika Bajeti yake. Korti zetu ni lazima zitapakae kila mahali mashinani. Katika Kilifi, watu hutembea kwa kilomita 50 ili wafike kortini. Hata yule ameshitakiwa kwa wizi wa kuku, kesi ambayo inaweza kumalizika mara moja, inabidi alipe nauli katika bas, matatu au boda boda ili kuhudhuria kesi yake kortini. Pesa ambazo zilikuwa zimepitishwa zilikuwa za ujenzi wa mahakama ili wananchi wapate huduma karibu kule mashinani. Je, mahakama ilifanya makosa gani iliposema kwamba Bunge likitaka kupitisha pesa za kaunti ni lazima mambo hayo yaende kwa Seneti? Mahakama haikufanya makosa yoyote. Kwa hivyo heshima ni lazima iweko kati yetu, Maseneta, na Wabunge wa Taifa, hasa nikizingatia kwamba hata Bibilia inatuambia kwamba Yesu aliulizwa na Mafarisayo ikiwa wangezitumia pesa hizo ambazo zilikuwa na picha ya kaisari kulipa ushuru kwa serikali au wazitumie. Yesu alisimama na kuangalia picha katika pesa hizo. Aliuliza: “Je, picha hii ni ya nani?” Alipoambiwa ni ya Kaisari, aliwaambia wale Mafarisayo: “Cha kaisari mpe kaisari na cha mwenyewe mpe mwenyewe.” Kwa hivyo, ikiwa uwezo wetu sisi ni kusema kwamba pesa zipewe serikali zetu za mashinani, hakuna ubaya. Tukisema vile vile kwamba ni vizuri ikiwa korti zetu zitakuwa na uwezo wa kupewa zile pesa na zitapakae mashinani, ili watu wasisafiri mbali The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}