GET /api/v0.1/hansard/entries/609967/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 609967,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/609967/?format=api",
"text_counter": 119,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "wakitafuta huduma za sheria, litakuwa jambo bora. Hata tunaambiwa vizuri sana katika Agano Takatifu kwamba: “Njooni tukae pamoja ili tuweze kuzungumza na kuelewana.” Najua kwamba hivi sasa kuna malumbano na kuamua “Nyumba kuu” kati ya Seneti na Bunge la Kitaifa ni ipi. Lakini hayo hayatatusaidia ikiwa tutalumbana. Malumbano sio maendeleo. Hatuwezi kukubaliana lakini tufanye kazi pamoja. Sisi tuko tayari kufanya hivyo. Hatufai kuwanyoshea kidole cha lawama ndugu zetu Wabunge. Nafikiria Kamati ambayo tutaunda itatekeleza wajibu wake ili kuona ya kwamba haki imetendeka. Sheria inafaa kuundwa kuhakikisha kwamba Seneti na Bunge la Kitaifa hazihusiki katika malumbano ambayo hayana suluhu. Asante sana, Bi. Spika wa Muda."
}