GET /api/v0.1/hansard/entries/609985/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 609985,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/609985/?format=api",
"text_counter": 137,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mositet",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 608,
"legal_name": "Peter Korinko Mositet",
"slug": "peter-korinko-mositet"
},
"content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ili nichangie Hoja hii. Kwanza, nawashukuru Wakenya kwa sababu mwaka wa 2010, waliweza kuzungumza na kuona kwamba kile kilichokuwa kinaturudisha nyuma ni Katiba tuliokuwa nayo wakati huo. Kwa sababu hiyo, tulipata Katiba mpya ambayo yapendeza na inampatia mwananchi wa Kenya nguvu. Namshukuru sana Spika na viongozi wetu wa Seneti kwa kuamua kwamba siku hii ya leo ni muhimu sana kwa Seneti kuzungumzia maneno muhimu. Ningependa pia kushukuru Kamati ya Fedha, Biashara na Bajeti inayohusika na bajeti hapa Seneti kwa sababu ilikaa chini, ikapitia Bajeti iliyopendekezwa. Waliona kwamba kulikuwa na umuhimu wa kaunti kuongezewa pesa. Kwa sababu hiyo, nashukuru na kusema kwamba hata baada ya malumbano na Kamati hiyo kuleta hoja hiyo katika Bunge la Seneti na hata tukapata Kamati ya Uwiano ya kuafikiana juu ya kiasi cha pesa ambazo zingeenda kwa kaunti zetu. Hata kama kila upande ulishikilia msimamo wake, wanakamati waliochaguliwa na Seneti walionyesha uzalendo kwani walielewa kilichowapeleka pale. Walikubaliana pesa hizo zipunguzwe hadi Kshs3 bilioni. Nawapongeza sana kwa hayo. Ninapongeza Mbunge aliyeweza kushikana na wawakilishi kutoka Seneti kwa kuona kwamba kulikuwa na Hoja. Bi. Spika wa Muda, hata kama Bunge la Kitaifa lilipunguza pesa hizo kutoka kwa Bajeti ya kitaifa kwa zile pesa ambazo Seneti na korti ingefaa kutumia, ni wazi kwamba pesa ziliweza kuongezeka kwenda kwa kaunti. Hongera kwa Seneti kwa sababu pale mbeleni wale Wabunge wa kitaifa hawakutaka kaunti ziongezewe hata ndururu. Hata The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}