GET /api/v0.1/hansard/entries/610138/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 610138,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610138/?format=api",
    "text_counter": 111,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Shukurani, Mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Ripoti ambayo imeletwa na Kamati hii ambayo inasimamia mambo ya jinsia. Ninawapongeza kwa kuwa Ripoti hii imetuonyesha waziwazi kuwa ni kweli kuna akina mama ambao wamepatiwa nafasi. Hata hivyo, kuna watu ambao hawako tayari kuwaona akina mama wakiongoza. Kwa sababu hiyo, kwa niaba ya akina mama wenzangu Kenya nzima, tunashukuru kwamba Kamati hii imemtoa mama huyu katika dhuluma ambayo alikuwa amepangiwa na wale wachache ambao hawataki kuona akina mama wakisonga mbele katika uongozi. Nawapongeza na naunga mkono Ripoti hii."
}