GET /api/v0.1/hansard/entries/610308/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 610308,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610308/?format=api",
"text_counter": 281,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Asante sana mhe Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niongee na kuwaunga wenzangu mkono kuhusu swala hili la CDF hapa nchini Kenya. Ni wazi kwamba labda watu wakiwa Nairobi hawawezi kujua hazina hii imefanya nini, haswa katika maeneo ya mashinani na mashambani, ambako kumekuwa na matatizo kwa muda mrefu sana. Mara nyingi pesa za kujenga shule zilikuwa zinategemea wananchi kufanya Harambee. Ilikuwa mara nyingi shule zinajengwa ovyo ovyo. Zinabomoka na zinaangukia watoto. Kwingine tumesikia kuwa watoto wamekabiliwa na vifo katika darasa kwa sababu ya shule ambazo zilijengwa kwa njia hafifu. Tangu hazina hii itengenezwe kupitia sheria za nchi hii wakati mhe Rais Kibaki alikuwa amechukua hatamu za uongozi wa nchi hii, tumeona shule zikijengeka kisawasawa. Wakati huo huo tumeona kuwa kumbe shule zinaweza kujengwa kwa gharama zinazofaa. Vile vile tumeona mahabara. Shule zilikuwa zinaendeshwa bila The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}