GET /api/v0.1/hansard/entries/610309/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 610309,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610309/?format=api",
    "text_counter": 282,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "mahabara yoyote. Zikiwa na mahabara sasa watoto wetu wanaweza kusoma masomo ya sayansi bila matatizo. Zahanati ambazo zilikuwa ziko mbali, tumeona zikikaribia wananchi, na wanaweza kupata matibabu kwa urahisi . Akina mama walikuwa wakijifungua njiani, na kuhatarisha maisha yao na maisha ya watoto waliobeba . Imekuwa wanaweza kufikia matibabu kwa haraka iwezekanavyo kwa sababu hazina hii imeweza kuwafanyia kazi. Ni ajabu kuwa majaji wanaweza kutoa uamuzi bila kufikiria yote yaliyotendeka kupitia hazina hii . Wanaweza kufanya uamuzi kuwa wananchi hawajapata faida kutokana na hazina hii. Mimi kwa upande wangu, ninafahamu kuwa kuna kaunti, lakini je zimeweza kufanya nini tangu zianze? Tunaingia mwaka wa tatu sasa tangu tuwe na kaunti, na hatujaona kazi ambayo zimefanya, kulinganishwa na hazina hii. Ni wazi kuwa mabilioni ya pesa yanapeanwa kwa magavana waweza kufanya kazi lakini je hiyo kazi inafanyika? Kwa hivyo, wakati majaji walipokuwa wanafanya uamuzi huu, wangelifikiria kwa sababu sheria zinatengenezewa binadamu na mwananchi mwenyewe ni lazima afaidike na sheria hizo. Sheria hazitengenezwi ili kusomwa tu kwenye vitabu halafu mwisho siziweze kutumika. Wakati hazina hii ya maendeleo ilipokuja, Taveta ilikuwa na shule tatu za sekondari ambazo hazikuwa hata na mahabara ya kuweza kuwafundishia watoto masomo ya sayansi. Leo hii nikiongea, shule za sekondari Taveta zimefika kumi. Zina mahabara na kila kitu ambacho ni cha kisawasawa.Akina mama walikuwa wakitembea zaidi ya maili 20 ili kuweza kufikia hospitali kuu ya Taveta. Leo hii kila mtu akitembea kilomita tano unakuta kuna mahali anaweza kupata huduma ya afya kwa urahisi. Akina mama walikuwa wakitembea kilomita nyingi ili kuweza kufika mahali kuna maji ya kunywa. Sasa hivi hazina hii imeletea watu maji nyumbani. Je, hao majaji wanaishi wapi? Wanaishi hewani ama wanaishi hapa nchini Kenya; hawafahamu vile hazina hii imefanyia watu kazi? Ni jambo la kusikitisha kuwa majaji wengi wanaotoka katika maeneo ya Bunge yenye matatizo kama lile langu; wamesahau kule walikotoka na sasa wanafikiri maisha yao ni ya Nairobi."
}