GET /api/v0.1/hansard/entries/610311/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 610311,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610311/?format=api",
"text_counter": 284,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukrani mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono kwamba CDF ibaki. Ningetaka nikichangia hii Hoja nianze kwa kuwauliza waheshimiwa Wabunge wenzangu maswali. Swali la kwanza, je wanaotengeneza sheria ni akina nani? Wanaotengeneza sheria za Kenya ni sisi hapa na sisi ndio tulitengeneza sheria ya CDF, na hivyo basi CDF lazima ibaki. Kwa hali na mali, CDF ibaki. Hii ni kwa sababu magavana hivi sasa wanazunguka; unasikia wameenda kufungua miradi. Wangefungua nini kama ingekuwa si CDF? CDF imetuwekea mashule. CDF imetuwekea zahanati. CDF imetuwekea wadi za akina mama ambazo magavana wanaenda kufungua. Ingekuwa si CDF, wangefungua nini?Hii ni kwa sababu katika hiyo miaka yao mitatu ambayo tumewamiminia pesa chungu nzima hakuna cha kutuonyesha. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}