GET /api/v0.1/hansard/entries/610469/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 610469,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610469/?format=api",
    "text_counter": 80,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "yao na inategemea kila kabila liliita Mau Mau yake nini. Waliyoyafanya hao wabeberu katika nchi hii na kuwadhulumu watu wa Kenya yalikuwa mabaya na mengi sana. Kwa mfano, waliwafunga mashujaa wetu, mmoja wao akiwa ni hayati mwanzilishi wa taifa hili Mzee Jomo Kenyatta. Itafahamika kwamba tukiongea juu ya mashujaa na dhuluma ambazo walifanya wabeberu, na tunataka fidia ilipwe ili kufidia wale ambao walipata madhara kutokana na wabeberu na mambo waliyofanya. Itakumbukwa kwamba wanawake wa nchi hii walifanya mambo mengi kupigania uhuru wa Kenya. Lakini mara nyingi, wanawake wamesahauliwa katika kufidia mashujaa. Itafahamika kwamba wanawake wengi waliwachwa na mzigo wa kulea familia, na baadaye kufanywa wajane, baada ya mabwana zao kuuawa. Pia, wanawake wengi ambao mabwana zao waliwekwa vizuizini walinajisiwa na maafisa weupe na kubebeshwa watoto weupe ambao leo hii hawana baba; sijui wanaitwa wa nani. Itafahamika kwamba baadhi ya taabu tulizonazo leo katika Kenya ni zile ambazo tumeridhi kutokana na ukoloni wa wabeberu, mojawapo ikiwa ni shida ya ardhi. Tukiongea juu ya shida ya ardhi, itafahamika kwamba hadi tunapoongea siku ya leo--- Ukitembea katika eneo la Laikipia, utapata kwamba 90 per cent ya ardhi bado inamilikiwa na watoto wajukuu wa waliokuwa wakoloni. Wenyeji wameachwa wakipigania vijipande vidogo sana vya ardhi."
}