GET /api/v0.1/hansard/entries/610494/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 610494,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610494/?format=api",
"text_counter": 105,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2715,
"legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
"slug": "esther-nyambura-gathogo"
},
"content": "Tunapoongea kuhusu mambo ya wazee ambao walipigania Uhuru wetu, inaonyesha kuwa kuna mambo ambayo yanafanyika katika nchi hii yetu ya Kenya. Kuna watu muhimu sana lakini mara kwa mara, wanasahaulika. Nimetoka katika Kaunti ya Kiambu lakini sina uhakika kwamba watu wote ambao walipigania Uhuru walipata fidia. Kwa sababu hapa hatugombani, ni ukweli kuwa kuna watu wengi ambao walipigania Uhuru, lakini ni wangapi ambao walipeleka kesi kortini na wakasaidika na ile fidia kidogo ambayo ilitolewa? Kwa hivyo, tunafaa kuungana kama Wakenya bila kusema ni kabila fulani ama nyingine ambayo ilipata hiyo fidia kidogo ambayo ilipatikana. La muhimu zaidi ni kuwa hatutaki kuwasahau hawa watu. Juzi, nilihudhuria mazishi ya cucu Mumbi, lakini ukiangalia hawa watu wamesahaulika. Hata kama ulipata hiyo pesa ama haukupata, la muhimu ni kuwa Serikali inawakumbuka hawa watu hata wakati wako nyumbani kwao. Ningeomba sisi wote kama Wabunge ambao tunawakilisha Kenya nzima tushikane pamoja ili tujue ni nani amewachwa nje na ni nani amesaidika. Tukikaa hapa, hatuwezi kujua ni akina nani wamewachwa. Kuna watu wengi katika Kenya ambao wakisikia kuwa kuna mahali ambapo kunapatikana pesa, wanajiita jina la Mau Mau na majina mengine kutoka kwa kabila tofauti. Tunafaa kuangalia ili tujue ni nani alipigania Uhuru na ni nani alikuwa katika mstari wa mbele. Tunafaa kuwa wavumilivu na tusichukulie kuwa Gitu Kahengeri aliwapeleka Wakikuyu ng’ambo ama mwingine alipeka watu kutoka kabila fulani. Tunafaa kushikana ndio kila mtu aweze kusaidika kwa sababu wote walitupigania. Watoto ambao wako nyuma yetu hawajajua jina “ Mau Mau” lina maana gani. Nikijua tulipiganiwa na tukashida, sitaki watoto wangu wajue maana ya “ Mau Mau .” Ninataka kuwaonyesha kuwa tuko katika nyakati zingine. Ni vizuri watoto wetu wasome kuhusu zile nyakati za zamani ili waweze kujua ile kazi ngumu ambayo ilifanywa katika taifa letu la Kenya. Ninaunga mkono na ninamshukuru sana Mbunge aliyeleta Hoja hii katika Bunge."
}