GET /api/v0.1/hansard/entries/610498/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 610498,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610498/?format=api",
"text_counter": 109,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Ni wajibu wetu sisi kama Waheshimiwa kwenda mashinani na kuleta rekodi kamili kwa maana kila mmoja wetu anamjua ni nani aliyeweza kusimama kidete katika sehemu yake ya uwakilishi na kutetea haki za Wakenya. Baadaye, tunapaswa kuwa na kamati maalumu ambayo itaisukuma Serikali yetu ili iweze kuwatetea watu wetu ili waweze kupata haki yao. Hata kama watu hao wameshakufa, wameacha watoto na wajukuu. Hatutakwenda tukamfukue mtu ndiyo aje aseme kwamba aliteswa, lakini tunawajua wale ambao waliteseka. Kwa hivyo, ni wajibu wetu, kama Waheshimiwa, kuchukua rekodi na kusimama imara kuwatetea hao ndugu zetu. Kutambuliwa tu kama mashujaa, haijatosha. Baadhi yao hawatambuliwi kamwe kama mashujaa. Wapeni kitu familia zao ishikilie, na ishukuru Mwenyezi Mungu kwamba kutoka na kizazi chao, wameweza kunufaika katika familia yao. Hoja aliyotuletea Bungeni mheshimiwa huyo siyo kana kwamba aliumia peke yake, lakini Mwenyezi Mungu amemuwezesha na kumpa moyo ili aweze kuileta Hoja hii Bungeni. Sisi, kama Waheshimiwa, tunaiunga mkono. Kwa niaba ya watu wa Kwale, ninampongeza na kumshukuru. Tuendelee kushikana mpaka Mkenya apate haki yake. Haki bado haijatendeka kwa wale ambao walipigania uhuru wa nchi yetu. Kuongezea, kuna maovu yaliyotendwa baada ya wakoloni kuondoka. Tunataka hayo maovu pia yafuatiliwe, haswa upande unaohusika na masuala ya ardhi. Suala la ardhi limeumiza watu. Mpaka sasa tunaishi kama maskwota licha ya kwamba tunasema tuko katika Kenya huru. Kwa hivyo, tunaiomba Wizara inayohusuka na masuala ya ardhi, pamoja na Tume, wajikakamue zaidi. Pesa tulipitisha tukawapatia. Tunachotaka ni kuona kwamba ardhi yetu imeregeshwa, na ardhi yenye utata ishuhulikiwe ili mwenye ardhi apewe ardhi yake bila kucheleweshwa. Ahsante sana, tunaishukuru Serikali yetu na kumshukuru sana mheshimiwa mwenzetu kwa kuileta Hoja hii Bungeni. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii."
}