GET /api/v0.1/hansard/entries/610515/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 610515,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610515/?format=api",
    "text_counter": 126,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wekesa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2742,
        "legal_name": "David Wafula Wekesa",
        "slug": "david-wafula-wekesa"
    },
    "content": "Asante sana kwa kunikabidhi fursa hii ili nami nichangie Hoja hii na kumpongeza Mheshimiwa Wangamati kwa kuileta. Mheshimiwa Wangamati ni mzee ambaye amekula chumvi nyingi sana na tunajua kwamba kuishi kwingi ni kuona mengi. Nina hakika Mheshimiwa Wangamati kwa kuishi kwingi aliwahi kukutana na baadhi ya hawa mashujaa na ni muhimu tumuunge mkono kwa Hoja hii . Ingawa tumesema kwamba kuna baadhi ya mashuja ambao watalipwa fidia, ni vyema tuhakikishe kwamba wanalipwa hizi fedha. Vile vile, tujue ni kiwango gani kitalipwa maanake huenda ikawa watalipwa pesa kidogo. Tunajua ya kwamba, kwa upande wa pesa Wakenya hawaeleweki. Huenda wanataka kuwatumia hawa wazee ili wafaidike wenyewe. Ni muhimu pia Serikali iingilie hili jambo ili iwape hawa mashujaa mawakili. Tunajua ya kwamba karibu nusu ya hizi fedha ambazo zinalipwa zinaenda kwa mawakili. Ingekuwa muhimu iwapo Serikali itaingilia hizi pesa za wakili sizikuwe nyingi ili ziweze kuwanufaisha hawa wazee. Vile wenzangu wamesema ni muhimu sana Serikali iweze kutambua hawa wazee ama mashujaa waliopigania Uhuru wa nchi hii. Tunajua kuna wazee kama Mheshimiwa hayati Martin Shikuku. Tunajua mambo ambayo alichangia akiwa katika Bunge hili na pia alipochangia wakati wa Lancaster. Lakini wakati alipoaga dunia, mambo mengi yaliongelewa wakati wa mazishi na kumbukumbu zake. Lakini baada ya hapo mengi yametupwa kwenye kaburi la sahau. Pia kuna mashujaa wengi ambao hatuwajui. Ingekuwa vyema iwapo Serikali ingechukua rekodi na kumbukumbu yote ili watoto wetu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}