GET /api/v0.1/hansard/entries/610532/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 610532,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610532/?format=api",
"text_counter": 143,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Chea",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1694,
"legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
"slug": "mwinga-gunga-chea"
},
"content": "Shukrani sana Bi. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Ningependa, mwanzo, nitoe shukrani zangu za dhati kwake mhe Wangamati kwa kuleta Hoja hii. Naiunga mkono Hoja hii kwa maana ni nzuri na imeletwa kwa wakati mwafaka. Upiganiaji uhuru katika nchi yetu haukuwa kazi ya mtu mmoja. Kazi hii ilifanywa na watu binafsi, jamii na taasisi mbali mbali. Ili tuweze kujua mambo yalivyojiri, kuna maswali ambayo lazima tuulize na tupate majibu. Swali la kwanza ni hili: Ni akina nani walipigania uhuru? Pili, katika kupiginia uhuru ni yapi mema na mabaya yaliyotokea? Je, hali ya maisha ya wapiganiaji huru leo hii iko vipi? Mwisho, ni lazima tujadili masuala ya malipo ya wapiganiaji uhuru. Swali la kwanza nimelijibu. Ukweli ni kwamba kuna jamii mbali mbali ambazo zilipigania uhuru wetu. Tulikuwa na kundi la Mau Mau, Dini ya Msambwa na makundi mengine kutoka sehemu nyingine humu nchini. Jamii ya Mijikenda inapatikana katika Mkoa wa Pwani. Katika jamii hii kuna watu ambao sisi tunajivunia kwa kuwa walipigania uhuru na wakatuletea mema. Kwa mfano, katika jamii ya Wagiriama kulikuwepo na mama shujaa aliyeitwa Mekatilili wa Menza. Yeye sifa zake zilivuma sana. Historia ya Kenya imemrekodi vya kutosha. Alipigania uhuru lakini hali ya maisha ya jamaa zake si nzuri. Katika eneo Bunge langu kuna mama anayeitwa Mepoho. Nimekumbushwa na mheshimiwa mwenzangu kwamba katika maeneo ya Rabai kulikuwa na mama aliyeitwa Mengao Mose, ambaye alikuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wetu. Mwingine anayejulikana ni Bi. Mtwana. Wote hawa walihusika. Kando na watu waliopigania uhuru, zipo taasisi ambazo zilipigania uhuru. Kwa mfano, katika jamii zetu zipo zile Kaya. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}