GET /api/v0.1/hansard/entries/610538/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 610538,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610538/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadime",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": "Shukran, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Mwanzo kabisa, Hoja hii ni muhimu sana maanake pembe zote za Kenya kwa muda mrefu watu huzungumza kuhusu hawa wazee wetu ambao walipigania Uhuru lakini hakuna mtu ambaye alijitokeza na kuleta hii Hoja Bungeni. Mheshimiwa Wangamati, nakupa kongole kwa Mungu kukumulika ili ulete hii Hoja hapa Bungeni. Wakenya ni kitu kimoja. Hata lile neno la umoja liko katika wimbo wetu wa kitaifa na limerejelewa. Hili neno lilitoka kwa sababu ya ule umoja Wakenya walikuwa nao wakipigania Uhuru. Ni vyema kuwafidia Mau Mau lakini pia ingekuwa vyema zaidi kama wale ambao walipigania Uhuru pembe zote za Kenya kufidiwa. Hata kuna wengine ambao walipigana vita vya ulimwengu na wamesahaulika kabisa. Hakuna jambo gumu kama kujitolea mhanga. Kule kwetu Taita Taveta kuna watu kama Mwangeka ambaye alijitolea mhanga. Ni vyema kumtambua kama mmoja wa wapiganiaji Uhuru. Vile vile, kuna mapango ambapo hata mwanzilishi wa taifa hili letu la Kenya, Mzee Jomo Kenyatta, alikuja wakati mapambano yalikuwa moto moto pande The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}