GET /api/v0.1/hansard/entries/610539/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 610539,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610539/?format=api",
    "text_counter": 150,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadime",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "hizi. Alikuwa anafichwa kwa hayo mapango. Ni vyema Serikali kutambua mapango hayo na wale ambao walihusika kuwaficha hawa wapiganiaji Uhuru. Kwa upande wa mashamba, ni kweli baada ya kupata Uhuru kuna wananchi ambao bado wanatatizika katika mashamba ambayo yalimilikiwa na hao mabeberu. Mwatate ni mojawapo ya mahali ambapo wanasumbua wananchi sana kwa mashamba. Ni vyema, baada ya kupitisha hii Hoja, tujaribu kuangalia kila mahali na tutengeneze ile kamati ambayo itafuatilizia hii Hoja na itekeleze kila kitu ambacho tunaongea hapa. Ni vyema kutambua yeyote ambaye amefanya kitendo cha ushujaa. Kama vile mwenzangu aliyenitangulia alisema, hawa wazee wa “Nyumba Kumi” na vijiji ni watu ambao wamesaidia kwa muda mrefu sana. Wangetambuliwa pia. Hata kule Taita Taveta kulikuwa na sherehe za kumbukumbu za Vita vya Kwanza vya Dunia. Wakati Vita vya Kwanza vya Dunia vilikuwa kule, baadhi ya watu ambao walikuwa wanaishi hapo walipelekwa mahali tofauti tofauti. Kwa hivyo, ni vyema kutambua watu hao na mahali kama hapo. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, mengi yameongelewa na sitakuwa na mengi ya kuongezea. Ninaunga mkono Hoja hii. Asante sana."
}