GET /api/v0.1/hansard/entries/610570/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 610570,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610570/?format=api",
    "text_counter": 181,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Maajabu yalifanyika. Haikujulikana vile wananchi walifanyiwa wakati huo. Haswa ukienda Samburu, kuna mzee mmoja kwetu anaitwa Leaduma. Ukitaka kumpiga mwanamke au mtoto unamwambia: “Nitakupeleka mahali Leaduma alipelekwa.” Lakini hatujui Leaduma alipelekwa wapi. Kwa hivyo, wale wenzetu waliopigania Uhuru wa Kenya, nafikiri ni Wakenya wote. Hakuna pembe haikuteswa ama kuwa na waliopigania Uhuru na kuteswa. Tuna mzee mmoja, marehemu, alikuwa anaitwa Lekalja. Ndiye alimlisha marehemu Jomo Kenyatta katika Samburu. Wakati alikuwa anaenda kupeleka maziwa ama nyama yake, ile taabu alipata ilikuwa ni ya maajabu sana. Hadi sasa, familia ya Lekalja ama familia ya Leaduma tunavyosikia bado wanafuata historia ya baba zao walivyofanyiwa."
}