GET /api/v0.1/hansard/entries/610574/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 610574,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610574/?format=api",
"text_counter": 185,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Kwa hivyo, Serikali ingeangalia wale mabeberu wamebaki hapa - hata kama wanasema wao ni Wakenya - bado wanawaona Wakenya ni kama wako katika ukoloni. Hii ni kwa sababu tunaona watoto wetu wakipigwa wakipatikana wakifuga ng’ombe katika mashamba ya wazungu. Bado unapigwa, unateswa na unapigwa risasi. Hakuna kitu hatufanyiwi wa wale walibaki. Kwa hivyo, ningetaka kusema warudishwe kwao. Bado tuna uchungu sana. Yangu ni kusema tu tunaunga mkono na tunamshukuru Mhe. Wangamati kwa kuleta Hoja hii. Napendekeza kamati iundwe kutoka Bunge ili izunguke na kuyachukua majina ya familia ya wale waliopigania Uhuru. Pia, wale waliopigana katika Vita vya Pili vya Dunia, wangewekwa pamoja kwa sababu hawajulikani. Wakati wa Mashujaa Day, ingefaa wale wamebaki wapewe nafasi ili wapate kujulikana hasa na watoto wa kisasa kwamba ndiyo walipigania Uhuru wetu. Mhe. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono. Ahsante."
}