GET /api/v0.1/hansard/entries/610612/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 610612,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610612/?format=api",
"text_counter": 223,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nassir",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kumshukuru mwenzetu Mhe. Wangamati kwa kuileta Hoja hii katika Bunge. Ningetaka kuipeleka Kenya katika mwaka 1913 ambapo katika maeneo ya Pwani, kulikuwa na mwanamke wa Kigiriama aliyejulikana kama Mekatilili wa Menza aliyekataa mila, desturi, uonevu na unyanyasaji wa Uingereza. Alikataa maonevu ya kiuchumi. Wakoloni walikuwa wakiweka kila aina ya ushuru katika biashara zao na kuathiri maswala mengi yakiwemo kulipa ushuru kwa kila nyumba almaarufu ikijulikana kama Hut Tax. Katika mwaka huu wa 1913, Mekatilili wa Menza, pamoja na mwenzake, Wanje wa Moderikola, walishikwa na kupelekwa hadi sehemu ya Mumias. Baada ya miezi, walitoka Mumias na walikimbia. Ni muhimu kuwa tukiwa wenye kuangalia maswala ya waliopigania Uhuru wa Kenya, tuhakikishe watakuwa wote ambao walipigania Uhuru huu katika Kenya."
}