GET /api/v0.1/hansard/entries/611763/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 611763,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/611763/?format=api",
    "text_counter": 156,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika, naomba nichukue nafasi hii nichangie Mswada huu, ambao umeletwa Bungeni kuhusu Mkaguzi Mkuu. Niko na mambo matano au sita ambayo ningeomba niyaangazie ili tupate mwelekeo unaofaa kuhusu Mswada huu, ambao umeletwa Bungeni. Kitu cha kwanza ni uhuru wa Mkaguzi Mkuu. Mkaguzi Mkuu ambaye anahusika na ukaguzi wa vitabu vyote, au hesabu zote za Serikali pamoja na mashirika ya Serikali, anahitaji kuwa na uhuru wa kuajiri wafanyikazi wake. Tukiangalia kipengele kimoja Tume ya Uajiri wa Umma, kwa kimombo “Public Service Commission” ndio inatakiwa kuajiri wafanyi kazi wa Mkaguzi Mkuu."
}