GET /api/v0.1/hansard/entries/611764/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 611764,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/611764/?format=api",
    "text_counter": 157,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Utakubaliana na mimi kuwa tukifuata mwenendo na mtindo huo, tutakuwa tunamnyima Mkaguzi Mkuu wa Serikali na mashirika yake uhuru wa kuwachagua wafanyikazi ambao anahitaji kulingana na vyeo, majukumu na sifa zao. Kama vitengo vingine vya Serikali vinaajiri watu wake vyenyewe, kwa nini tumnyime Mkaguzi Mkuu wa Serikali uwezo huo? Maoni yangu ni kuwa apatiwe uhuru wa kuwaajiri wafanyikazi wake kulingana na uwajibikaji wa ofisi yake. La pili ni kiapo. Mkaguzi Mkuu anahitajika kula kiapo mbele ya Mkuu wa Sheria. Kwa nini aapishwe mbele ya Mkuu wa Sheria? Kwa nini asiapishwe mbele ya Rais? Haieleweki ni kwa nini aapishwe huko. Kwa nini asikichukue kiapo chake mbele ya Rais? Naomba tuyachunguze mambo haya ili tuone ni vipi tunavyoweza kumfanya Mkaguzi Mkuu awe na uhuru, aonekane kuifanya kazi yake bila upendeleo na bila kufuatiliwa ama kuwa na uoga. Jambo lingine ambalo ningeomba kuangazia ni makadirio. Hivi sasa, inabainika wazi kuwa inambidi Mkaguzi Mkuu kupeleka makadirio yake kwa afisa anayehusika na fedha kwenye Hazina ya Kitaifa. Kwa nini ayapeleke huko? Kwa nini haya makadirio yasiletwe Bungeni kama ana uhuru wake? Hii itampatia Mkaguzi Mkuu nafasi ya kufanya makadirio yake, kuyaleta Bungeni kama vile sisi tunayafanya yetu na kama vile wanasheria wanaleta yao wenyewe. Kwa nini alazimishwe kuyapeleka makadirio yake kwa kitengo cha fedha ambacho yeye mwenyewe ndiye anakikagua? Inabainika wazi wazi mara nyingi kuwa akiomba kuongezewa fedha, fedha zake zinapunguzwa ili asije akawa na nafasi ya kuchunguza mashirika yote pamoja na Hazina ya Kitaifa. Kila wakati, Hazina ya Kitaifa inapunguza fedha za Mkaguzi Mkuu ili isipate nafasi ya kufanya ukaguzi wa kutosha. Kama itawezekana--- Niko na imani itawezekana kwa sababu nimemsikia mwenyekiti wa kamati ambayo inahusika na jambo hili, mhe. Langat, ambaye alikuwa hapa, akisema kuwa atapokea na atakubali mapendekezo ambayo yatatoka kwa umma pamoja na sisi Wabunge ambayo yatapendekeza kuwa Mkaguzi Mkuu apatiwe uhuru wa kutekeleza wajibu wake kama vile Katiba inavyomhitaji. Jambo lingine ambalo ningependa kuchangia ni kuhusu majukumu ya Mkaguzi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}