GET /api/v0.1/hansard/entries/611765/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 611765,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/611765/?format=api",
"text_counter": 158,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mkuu. Majukumu haya yameongezeka. Hivi sasa tuna Serikali za ugatuzi 47, na zote zinahitaji kuangaliwa na Mkaguzii Mkuu. Fedha ambazo amepatiwa ni zile zile alizokuwa akipatiwa wakati hatukuwa na Serikali za ugatuzi. Tuulizane wazi: Je, hiyo ni haki? Hawezi kuifanya hii kazi kama ana fedha zile zile ambazo alikuwa nazo wakati ambapo hatukuwa na Serikali za ugatuzi. Kuna mashirika mengi ambayo yameundwa. Kuna ile hazina ya maeneo ya uwakilisha Bungeni ambayo tunaiita CDF. Mkaguzi Mkuu anahitajika kufanya ukaguzi huko, na fedha ambazo anazo ni zile zile ambazo alipangiwa. Tumeunda mashirika mengi na yote yanahitaji ukaguzi wa vitabu kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Hataweza kuifanya kazi hii kama hataongezewa fedha. Kama makadirio yake yatapitia katika Hazina ya Kitaifa, ninasikitika na nina uoga na wasiwasi kuwa hatapatiwa fedha ambazo ataomba. Makadirio yake na ombi lake yanafaa kuja moja kwa moja Bungeni, ili yashughulikiwe na Bunge. Yeye atakuwa na uhuru wake na sisi tutapata muda wa kuchangia na kumuuliza “Hizi fedha unazoziomba, ni za kufanya kazi again?” Yeye ataijibu kamati ya Bunge na kuieleza vile anavyotaka kuutekeleza wajibu wake. Hapo, tutamsaidia na kumpatia peza za kutosha ili kuwajibika. Lakini ikiwa ni lazima apitie katika Hazina ya Kitaifa ninasikitika kwamba hataweza kupata kile atakachohitaji. Nikiongea kuhusu usalama, mara nyingi tumeambiwa Mkaguzi Mkuu hawezi kukagua vitu ambavyo vinanunuliwa na ambavyo vinahusu usalama wa nchi. Hapo ndipo kuna ufisadi wa hali ya juu. Pendekezo langu ni kuwa aruhusiwe kukagua na akitoa ukaguzi wake, si lazima huo ukaguzi uchambuliwe ama uwekwe hadharani. Unaweza kupelekwa kwa Rais kwa sababu hata Rais angependa kujua ni mambo gani ambayo yanatokea katika mashirika, hasa katika mashirika ambayo yanahusika na usalama. Kwa mfano, jeshi letu linanunua vifaa ambavyo vinahitajika. Lakini tukiangalia vile Mswada huu umeletwa, kuna pahali ambapo wanataka kujikinga kabisa na vitabu vyao visichunguzwe. Je, nani atagundua kama kuna ufisadi kama hatutamtarajia Mkaguzi Mkuu aangalie hivyo vitabu na angalie fedha za umma zimetumiwa namna gani? La mwisho, ni sikitiko kuona kuwa kila mwaka na kila muhula, Mkaguzi Mkuu akitoa ripoti yake, inaletwa Bungeni. Inaenda kwa Kamati mbalimbali, wanazijadili na kisha wanatoa maoni yao na wanapitisha maamuzi. Maamuzi haya yakipitishwa, hayatekelezwi. Utaona kwamba wanaohusika wanaachwa na wanaofanya wizi wanawachwa. Hawashughulikiwi. Wakati huu, kwa sababu tunakuja na sera na uwajibikaji mpya wa ukaguzi, ripoti yoyote ya Mkaguzi Mkuu ikiletwa Bungeni, tukiipitisha, wale ambao hawajatekeleza majukumu yao kulingana na ripoti ya Mkaguzi Mkuu, basi wachukuliwe hatua. Wasiachwe waendelee hivi hivi. Inaonekana ni fedheha. Mwaka baada ya mwaka, ripoti zinakuja hapa Bungeni, tunazichangia, tunazizungumzia, tunatoa mapendekezo yetu na baada ha hapo mambo yanakwisha. Ripoti inawekwa kwa kabati, inaokota vumbi, inaliwa na panya na kombamwiko wanailalia. Tunafaa kusisitiza na kuweka wazi kuwa wakati huu ripoti ya Mkaguzi Mkuu ikipitia Bungeni, itatekelezwa."
}