GET /api/v0.1/hansard/entries/611931/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 611931,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/611931/?format=api",
    "text_counter": 324,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Lay",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1022,
        "legal_name": "Joyce Wanjalah Lay",
        "slug": "joyce-wanjalah-lay"
    },
    "content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Pia namshukuru Mhe. Okoth kwa kuleta Hoja hii kwa sababu ni jambo ambalo limetutatiza sana. Wakati umefika ambapo elimu yetu ya Kenya iweze kupigiwa msasa kamili kwa sababu kunayo matatizo mengi yameikumba, kuanzia wanafunzi mpaka wale ambao wanawaangalia kama vile wazazi au wale ambao wanawachunga. Kuanzia mambo ya kulipa karo na vilevile kuangazia mambo ya vile uchaguzi unaofanywa watoto wakienda katika kidato cha kwanza, unapata kwamba kuna kuwa na ubaguzi sana wakati wa kuchagua wanafunzi ambao wataenda katika kidato cha kwanza, na hii imeleta kero sana kwa wazazi ambao wanataka elimu bora katika maisha ya watoto wao. Tukiangazia mambo ya kulipa karo, ni kwamba jambo hili limekuwa jambo zito sana haswa kwa wananchi wa kawaida wa Kenya. Pesa ambazo tunalipa kama wazazi ni nyingi mno. Mimi kama kiongozi anayesimamia kaunti yote nzima, sina kitengo ambacho kimetengwa kama CDF ama“bursary”, lakini kila mwaka lazima niandike cheki ya Kshs.800,000 ili watoto waweze kusoma. Unapata kwamba wanaopata mzigo huu sana sana ni wanawake. Wanawake wanaumia katika mambo ya kulipa karo za watoto. Ni kitu ambacho kinaumiza sana wakati pia akina mama wanatukanwa wakiambiwa: “Kwani hawa walimu ni wa mama yako”. Hilo ni jambo la kushangaza - kwamba hata sisi akina mama hatupatiwi heshima na sisi ndio tunaumia na kubeba mzigo wa wanafunzi ili waweze kusoma. Tukiangazia pia katika mambo ya walimu, wamekuwa kila mwaka wanaandamana.Wakati umefika sasa kwa Serikali, viongozi na wanaoshughulika mambo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}