GET /api/v0.1/hansard/entries/611932/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 611932,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/611932/?format=api",
"text_counter": 325,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Lay",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1022,
"legal_name": "Joyce Wanjalah Lay",
"slug": "joyce-wanjalah-lay"
},
"content": "ya elimu kuketi ili jambo hili liweze kutatuliwa mara moja ili watoto waweze kusoma. Hii ni kwa sababu tunawanyima watoto haki yao ya kupata elimu. Kwa hivyo, katika mambo ya karo, ni lazima tuketi tuweke vichwa pamoja na tuhakikishe kwamba wanafunzi wanaweza kupata haki yao ya kusoma. Vile vile, naangazia pia wanafunzi ambao hawapati zile alama za kuweza kwenda kidato cha kwanza. Kama mwaka jana, kuna watoto 2,000 ambao hawakuweza kwenda kidato cha kwanza kwa sababu hawakuweza kupata ile alama ya 200. Ni lazima tuketi chini tuangazie jambo hilo hili tusiwanyime watoto haki yao. Watoto wa miaka 13, tunasema waende “polytechnic”. Hakuna mikakati tumeweka ya kuhakikisha kwamba watoto wameenda “polytechnic”. Wengi wanaingilia mambo ya madawa ya kulevya na kufanya ukahaba. Kwa hivyo, ni lazima tuweke vichwa vyetu pamoja ili tuweze kulitatua jambo hili. Ahsante sana."
}