GET /api/v0.1/hansard/entries/611969/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 611969,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/611969/?format=api",
"text_counter": 362,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nassir",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kusema kwamba sauti ya Bunge hili ni sauti ya Wakenya. Rai yangu kwa wakuu wa elimu ni kwamba wazibebe sauti zetu wakijua kwanba wamebeba maoni ya Wakenya na sauti ya kila mmoja alioko hapa ambaye amezungumza kwa bughutha kuhusu hali ya elimu ilivyo; hususan, masuala ya karo katika shule za upili. Serikali ilikaa na ikatengeneza Ripoti ambayo ilipeana. Ripoti ya Jopo lililoongozwa na Kilemi Mwiria iliandika kwa umakinifu kwamba: Kama sekta ya elimu nchini ingepewa Kshs11 bilioni, basi kila asomaye katika shule ya upili atasoma bure, isipokuwa wale wasomao katika shule za malazi, ambao watalipa Kshs38,969. Naikumbusha nchi hii na Serikali kwamba Kshs11 bilioni ni asilimia 0.55 ya Bajeti ya Kenya ya trilioni mbili. Ikiwa hatuwezi kusema kuwa tunachukua asilimia 0.55 ya Bajeti ya Kenya kwa sababu ya kujali masomo ya watoto wetu, basi tutakuwa tunaelekeza nchi hii kwenya mrengo usioeleweka. Kenya iko katika hali ya kipekee katika dunia hii ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu wanalipa gharama za chini kuliko wanafunzi katika shule za upili. Nataka tuweke wazi kuwa kama Serikali haitahakikisha kwamba ahadi iliyowekwa na viongozi wa zamani na wa sasa - kwamba fedha hizo zitawekwa - na ikiwa Bunge hili halitaweza kutenga Kshs11 bilioni ili wanafunzi wetu wasome, basi tutakuwa tunapitisha mabilioni ya kujenga majumba ya mahabusu zaidi kwa sababu tutakuwa, badala ya kujenga wanafunzi---"
}