GET /api/v0.1/hansard/entries/612029/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 612029,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/612029/?format=api",
    "text_counter": 422,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wekesa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2742,
        "legal_name": "David Wafula Wekesa",
        "slug": "david-wafula-wekesa"
    },
    "content": "Bwana Naibu Spika wa Muda, mimi nashangaa sana. Juzi, Waziri wa Elimu alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba iwapo kuna mtu ana habari kwamba shule fulani inaitisha karo zaidi ya kiwango ambacho kiliwekwa, amjulishe. Hilo si jambo la kujulishwa. Ni wazi linafanyika. Ni wajibu wake kuhakikisha kwamba shule zinaitisha pesa zinazofaa. Kuhusu pesa za mtihani, tunajua ya kwamba Serikali ilitangaza wazi msimamo wake. Ingawa hivyo, kuna walimu fulani wanaitisha pesa za mtihani. Ni wajibu wa Waziri wa Elimu kuwafikia walimu kama hao na kuwaeleza kwamba kufanya hivyo siyo haki. Wengi wameongea kuhusu Ripoti ya mheshimiwa Kilemi Mwiria ambaye alikuwa Mbunge hapo awali. Wakati umewaadia kwa Waziri kutekeleza ripoti hiyo. Asipofanya kitu, wanafunzi wengi ambao wanatoka jamii maskini hawatasoma."
}