GET /api/v0.1/hansard/entries/612470/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 612470,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/612470/?format=api",
    "text_counter": 172,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ningependa kuuliza taarifa kutumia Kanuni ya Seneti No.45, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo kuhusiana na maswala yafuatayo:- 1. Je, ni kwa nini mtambo wa Shirika la Kenya Cashew Nuts Limited, uliokuwa mikononi mwa chama cha ushirika, yaani Kilifi Cooperative Society, ulipewa Millennium Management Limited? 2. Je, ni nani aliyechukuwa alisimia 35 za hisa za wakulima wa Kaunti ya Kilifi? Je, hisa hizo za wakulima ziko wapi kufikia sasa? 3. Je, wakulima hao watarejeshewa lini hisa hizo, kwa sababu bado wako hai na wanaishi katika hali ya walalahoi? 4. Je, hayo mageuzi ya ununuzi wa shirika la Kenya Cashew Nuts Limited yalifanywa kulingana na sheria za Kenya? 5. Je, ni nani alitoa uwezo wa kuuza hisa hizo za Serikali au kutoa asilimia 65 za hisa kwa Kenya Assets Management Limited? 6. Ikiwa Millennium Management Limited ilinunua mtambo wa Kenya Cashew Nuts Company Limited pekee inaonekana wazi kwamba kampuni hiyo haikununua hektari 350 za shamba ambako kampuni hii ilijengwa. Je, Serikali itarejesha lini hizo hektari 350 za shamba kwa wananchi wa Kaunti ya Kilifi? 7. Je, Serikali ina mikakati gani kuhusu mtambo wa Kenya Cashew Nuts Company Limited pamoja na shamba lake la hektari 350 kurudishiwa wananchi wa Kaunti ya Kilifi?"
}