GET /api/v0.1/hansard/entries/615165/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 615165,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/615165/?format=api",
"text_counter": 1010,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Pia nami naunga mkono Hoja hii. Natoa shukrani kwa wenzangu kwa ile kazi nzuri wamefanya mwaka huu. Vile vile, Kenya imepata majanga; kumekuwa na shida Garissa ambapo tulipoteza wanafunzi wengi. Kenya pia imekuwa na matatizo mengine mengi. Lakini juu ya hapo mwaka huu tumepata baraka. Tumepata Rais Obama pamoja na Baba Mtakatifu wa Kikatoliki aliyekuja nchi yetu. Nataka kuwaombea Wakenya heri njema ya Krismasi na Mwaka Mpya ulio na mafanikio. Vile vile, nawaomba wenzangu wanapokwenda, waeneze habari njema ya upendo na umoja. Tusimame kidete kama Wakenya tukifurahia nchi yetu. Asante sana."
}