GET /api/v0.1/hansard/entries/615500/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 615500,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/615500/?format=api",
    "text_counter": 92,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kusema kongole kwa dada yangu Mhe. Amina na Wizara husika kwa kuleta sera ya kuhifadhi sehemu ya chemichemi. Wakenya wanakumbuka tulipopigana vita na kampuni ya Mumias Sugar walipotaka kuichukua Tana Delta kwa minajili ya kupanda miwa. Wachache tulisimama na tukasema kuwa chemichemi zinastahili kuhifadhiwa wala sikugeuzwa kuwa shamba la miwa. Iwapo tungekuwa na sera hii siku hizo, basi hatungezozana na kampuni ya Mumias Sugar. Kwa hivyo, nitampongeza Mhe. Amina na Wizara husika kwa kuileta sera hii ili chemichemi nchini zipate hifadhi. Chemichemi kubwa zaidi katika nchi ya Kenya iko katika Kaunti ya Tana River. Wakati tunapokuja na hizi sera na sheria, ni muhimu kukumbuka mila na desturi ya watu wanaoishi katika sehemu hizo. Hii ni kwasababu iwapo mwananchi atamiliki sehemu hizo, ni rahisi chemichemi kupata hifadhi kuliko kutumia nguvu. Natumai sera hii imehusisha serikali za ugatuzi pia ziweze kuchangia katika kuhifadhi chemichemi. Kwa hayo machache, naunga mkono sera hii."
}